Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkalama Bi Elizabeth Rwegasira akimwaga mchanganyiko wa Saruji na Kokoto kama ishara ya Ujenzi wa Nyumba ya Watumishi wa Kituo cha Afya cha Knyambuli |
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Mhandisi Jackson Masaka akimkabidhi mmoja wa wazee wa kijiji cha Kinyambuli Mche wa Sabuni ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 41 ya Chama cha Mapinduzi. |
‘’Una Chakula kitamu kiasi gani nyumbani kwako mpaka mtoto
wako asile na wenzake shuleni?’’
Hilo ni swali lililoulizwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe.
Mhandisi Jackson Masaka alipoalikwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Mgeni Rasmi
kwenye maadhimisho ya miaka 41 tangu kuzaliwa kwa chama hicho yaliyofanyika
Kiwilaya katika Kijiji cha Kinyambuli.
Mhe. Masaka amewasisitiza wazazi na walezi wote kuwa Msimamo
wa Wilaya ya Mkalama ni watoto wote wapate chakula shuleni kwa sababu Wilaya
imedhamiria kupandisha kiwango cha Ufaulu hivyo ni lazima wanafunzi watumie
muda mwingi kufundishwa na kusoma shuleni.
‘’Mhe. Rais hajakataza michango shuleni isipokuwa ameondoa jukumu la kukusanya
michango hiyo kwa walimu ili wajikite zaidi kutoa taaluma na si vinginevyo
hivyo ninaagiza kuanzia sasa ni marufuku kwa mzazi au mlezi kwenda shuleni
kudai kurejeshewa chakula alichokuwa ametoa kwa ajili ya mtoto wake”.
Amesisitiza Mhe. Masaka.
Katika hatua nyingine Mhe. Masaka amesema kuwa Serikali ya Awamu ya tano imefanya mambo
mengi sana na ya Msingi Wilayani Mkalama ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa daraja la
kisasa la Sibiti linalotarajiwa kukamilishwa hivi karibuni, Ujenzi wa madarasa,
bwalo na mabweni katika shule ya Sekondari Iguguno uliyoifanya Shule hiyo kuwa
ya kwanza kuwa na wanafunzi wa kidato cha tano na Uboreshaji wa Kituo bora na
cha Kisasa cha Kinyambuli.
“Rai yangu kwenu wananchi wa Kinyambuli naomba muwe
wazalendo juu ya mradi huu na msiukwamishe kwa namna yoyote kwa sababu pamoja
na kuwanufaisha wakazi wote wa Mkalama, nyie mnabaki kuwa wanufaikaji wakuu
kutokana na mradi huu kujengwa katika kijiji chenu” Amesisitiza Mhe. Masaka.
No comments:
Post a Comment