Afisa tarafa ya Mwangeza Ndugu Edward Makala akitoa utambulisho mfupi wa serikali ya kijiji kwa Mkuu wa Wilaya Mkalama Mhe: Christopher Ngubiagai (aliyekaa) |
Kaimu Afisa Ardhi wa Wilaya, Imikigwe Mwanitu (aliyevaa fulana ya bluu) akisikiliza kwa makini maswali na kero za wanakijiji wa Hilamoto zinazohusiana na Ardhi. |
Wanawake wa jamii ya kimang'ati ambao pia ni sehemu ya jamii ya wakazi wa kijiji cha Hilamoto wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe: Christopher Ngubiagai (hayupo pichani). |
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe: Christopher Ngubiagai akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Hilamoto kuhusiana na kero zao za masuala ya ardhi alipofanya ziara wikiendi iliyopita. |
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe: Christopher Ngubiagai
amewataka kutouza maeneo wanayomiliki kinyemela bila kupata ushauri kutoka kwa
wataalam kwa sababu jambo hilo ndio linalozalisha migogoro mikubwa ya ardhi
iliyopo hivi sasa.
Ngubiagai aliyasema hayo alipoenda katika kijiji cha
Hilamoto kilichopo Wilayani hapa ambako kuna mgogoro wa ardhi kati ya
Wanakijiji wa Hilamoto na mwekezaji anayefahamika kwa jina la Eugine Afrika.
Katika mgogoro huo wanakijiji wa Hilamoto wanamtuhumu
mwekezaji huyo kumiliki ekari 500 za Kijiji hicho bila makubaliano yoyote na
wanakijiji hao na badala yake aliwasilisha hati ya mahakama inayowataka
wanakijiji hao kumpa Afrika kiasi hicho cha Ardhi.
“Niliagiza huyo Mwekezaji alete nyaraka zinazozibitisha
umiliki wake wa hiyo ardhi lakini badala yake nikaletewa nakala ya hukumu
ambayo inaonesha alishinda kesi iliyofunguliwa kupinga umiliki wa ardhi hiyo
hivyo nilishindwa kuchukua hatua yoyote kwa sababu siwezi kuingilia au kupinga
maamuzi ya mhimili wa mahakama” Alisema Ngubiagai.
Badala yake, Ngubiagai aliwashauri wanakijiji hao
kuwasiliana na ofisi ya Mwanasheria wa Wilaya ili aweze kuwashauri namna ya
kulishughulikia suala hilo jambo hilo lifanyike kupitia muhtasari kamili wa
mkutano wa kijiji hicho.
Aidha Ngubiagai aliwatahadharisha wanakijiji hao
kuhakikisha kuwa hakukuwa na namna yoyote ya uuzaji wa ardhi hiyo ili kupata
nguvu ya malalamiko yao vinginevyo jitihada hizo hazitazaa matunda yoyote na
badala yake wanakijiji hao watapoteza pesa na muda wao.
“Kumekuwa na
utaratibu wa wanakijiji kuuza maeneo wanayomiliki bila kufuata utaratibu
wowote, matokeo yake wakiona yule waliyemuuzia anatengeneza faida kubwa kupitia
maeneo hayo wanaanza kulalamika kuwa wamedhulumiwa maeneo yao, tabia hiyo
muache mara moja” Aliongeza Ngubiagai.
Kuhusiana na mgogoro wa mpaka wa Mlima Dominiki
unaohusisha Wilaya ya Mkalama na Mbulu, Ngubiagai alisema kuwa amemuandikia
barua Mkuu wa Wilaya Mbulu ili waweze kukaa kikao cha ujirani mwema na
kuzungumza kuhusiana na hilo lakini bado hajapata majibu ya barua hiyo lakini
amemuandikia barua nyingine hivyo anasubiri majibu.
Hahahahaha, Naona Kaimu Afisa Ardhi katika umakini mkubwa... All in all keep up a good work son.. SALUTE
ReplyDeleteHadi na mi nakuona afisa ardhi
DeleteHadi na mi nakuona afisa ardhi
Delete