Idara
ya Mifugo na Uvuvi inatekeleza shughuli zake kwa kuzingatia sera ya Uvuvi ya
mwaka 2003 na Sera ya mifugo ya mwaka 2006 ambayo inasisitiza ufugaji wa
kibiashara wenye tija na ushindani wa kimataifa katika Uvuvi na ufugaji. Kuunga
mkono wafugaji wadogo ili waweze kuwa wajasiriamali wazuri. Vilevile kuwa na
matumizi endelevu ya rasilimali za Mifugo na Uvuvi ili kuwa na matumizi
endelevu ya rasilimali hizo.






Pia
pamoja na mambo mengine ina jukumu la kuimarisha huduma za kiuchumi kwa jamii
ili iweze kuwa na maisha bora na kufikia malengo ya MKUKUTA, Millenia na
hatimaye Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025.
MAWASILIANO:
JINA
|
NAFASI/CHEO
|
NAMBA YA SIMU
|
ELIAS E.MBWAMBO
|
MKUU WA IDARA
|
0789111720
0765028840
|
ABDALAH KHAMIS
|
AFISA UDHIBITI WA MAGONJWA/ MAJOSHO NA UKAGUZI WA NYAMA
|
0786347317
|
ABRAHAM MRINDOKO
|
AFISA MINADA
|
0788908933
|
BENEDICTO MABUBI
|
AFISA UVUVI
|
0758506008
|
2. TAKWIMU ZA IDARA
S/N
|
AINA YA
WANYAMA
|
IDADI
|
1
|
Ng’ombe
|
126434
|
2
|
Mbuzi
|
104335
|
3
|
Kondoo
|
47,720
|
4
|
Punda
|
6202
|
5
|
Nguruwe
|
3518
|
6
|
Kuku
|
303402
|
7
|
Mbwa
|
9529
|
3. MIUNDOMBINU
S/N
|
MAJOSHO
|
VITUO VYA AFYA YA MIFUGO
|
MINADA
|
MALAMBO
|
MABANDA YA NGOZI
|
MASHAMBA YA MIFUGO
|
1
|
21
|
6
|
9
|
15
|
3
|
1
|
Idadi
ya Kaya za wafugaji 12,645
4. MALENGO
YA IDARA
Katika
kipindi cha 2015/16 hadi 2016/17 Idara inategemea kuendelea kutoa huduma zake
ikiwa ni pamoja na Elimu kwa wafugaji,juu ya utengaji wa maeneo ya malisho na
kuyaendeleza. uboreshaji koosafu za mifugo pamoja na miundo mbinu ya huduma za
mifugo. pia ufugaji wa samaki Tiba,
Kinga kwa mifugo yote pamoja na kuboresha mifugo iliyopo kama ratiba
iliyoambatanishwa inavyoonyesha:
RATIBA YA
KINGA YA MAGONJWA YA MIFUGO KWA MSIMU WA MWAKA 2016 WILAYA YA MKALAMA.
UGONJWA
|
JANUARI
|
FEBRUARI
|
MARCH
|
APRIL
|
MEI
|
JUNI
|
JULAI
|
AGOST
|
SEPTEMBA
|
OKTOBA
|
NOVEMBA
|
DESEMBA
|
MDONDO (NEWCASTLE)
|
||||||||||||
KICHAA CHA MBWA (RABIES)
|
||||||||||||
CHAMBAVU NA VIVIMBE VYA NGOZI (BQ &
LUMPY SKIN)
|
||||||||||||
UOGESHAJI (DIPPING)
|
||||||||||||
DAWAYA MINYOO (DEWORMING)
|
||||||||||||
MAFUNZO NA MIKUTANO(TRAINNING AND
MEETINGS)
|
5.
MAFANIKO
i.
Utoaji wa Elimu na kufanya
mikutano mbalimbali ambayo imechangia kuleta mahusiano mazuri kati ya Idara na
Wananchi na ndiyo siri kubwa iliyowezesha kufanikisha malengo tuliyoyapanga.
ii.
Ushirikishwaji wa sekta
binafsi katika kuandaa na kutekeleza majukumu ya Idara kumechangia kufanikisha malengo
hayo ikiwa ni pamoja na kutoa Elimu, kutoa dawa za chanjo na kusaidia gharama
za uendeshaji wa jumla wa huduma ya kinga ya mifugo ndani ya Wilaya. Wadau hao
ni pamoja na Full Dimmension, Arusha Seed Co LTD, Alpha Vety, na TVLA.
iii.
Idara imefanikiwa kudhibiti
magonjwa ya mifugo kwa kutoa chanjo na kuogesha mifugo yote ndani ya Wilaya
kiasi cha kupunguza vifo vitokanavyo na magonjwa ya Kideri kwa Kuku, Lumpy
skin, Chambavu, na Ndigana Kali(ECF) kwa asilimia 85 (85%)






iv.
Katika kutekeleza ratiba
yetu ya mwaka 2016 imefanyika chanjo ya Mbwa na Kuku kwa awamu ya kwanza kama
ifuatavyo
S/N
|
AINA YA CHANJO
|
MIFUGO
|
LENGO
|
CHANJWA
|
% YA UTEKELEZAJI
|
MAELEZO
|
1
|
LSD
|
Ng’ombe
|
126434
|
-
|
0
|
Uchanjaji
haujaanza
|
2
|
PPR
|
Mbuzi
|
104335
|
-
|
0
|
Uchanjaji
haujaanza
|
Kondoo
|
47720
|
-
|
0
|
Uchanjaji
haujaanza
|
||
3
|
Newcasttle
|
Kuku
|
303402
|
233620
|
77
|
-
|
4
|
Rabbies
|
Mbwa
|
9529
|
2365
|
25
|
Chanjo inaendelea
|
CHANGAMOTO
·
Mwamko mdogo wa wananchi katika kuchangia ukarabati wa miundo
mbinu ya mifugo katika maeneo yao.
·
Uhaba wa vitendea kazi kwa wataalam katika kusimamia na
kutekeleza majukumu ya Idara kama vile usafiri.
·
Kutokupewa bajeti tunayoiomba kwa ajili ya utekelezaji wa
shughuli za
Idara ikiwemo ununuzi wa madawa
mbalimbali na vifaa vya kufanyia kazi.
·
Idara kutopewa 15% ya mapato yatokanayo na mapato ya Mifugo
na Uvuvi ambayo husababisha kutokuwepo kwa uendelevu wa sekta hii.
·
Mwamko mdogo wa wafugaji juu ya kukinga Mifugo yao kwa njia
ya chanjo na uogeshaji.
·
Serikali za Vijiji kutokuzingatia mgawanyo wa matumizi bora
ya ardhi kwa kutenga maeneo ya kilimo, ufugaji makazi na huduma mbalimbali za
jamii.
UFUMBUZI
1.
Kuendelea kuhamasisha wananchi kutoa michango kwa ajili ya ukarabati
wa miundo mbinu ya mifugo katika maeneo yao.
2.
Kupatiwa vitendea kazi na madawa ili kufanikisha utoaji wa
huduma kwa wafugaji.
3.
Kutengewa bajeti ya Idara ya Mifugo kama Idara ya kiuchumi
tuliyoiomba kwa ajili ya kufanikisha utoaji huduma mbalimbali kwa wafugaji.
4.
Idara kutengewa na kupewa 15% ya mapato yatokanayo na mapato
ya Mifugo/Uvuvi
5.
Kuendelea na juhudi za makusudi kuelimisha wafugaji juu ya
umuhimu wa kukinga Mifugo yao dhidi ya magonjwa hatari ya kuambukiza na kutoa
kinga kwa njia ya kuogesha mifugo.
6.
Serikali za vijiji zinashauriwa kutenga maeneo maalum kwa
ajili ya malisho ya Mifugo ili kuondoa uwezekano wa kuzuka kwa migogoro kati ya
wakulima na wafugaji katika maeneo yao na kuheshimu maeneo yaliyotengwa kwa
ajili ya huduma za Mifugo mfano minada, majosho, mapalio, malambo, vituo vya
huduma za Mifugo na maeneo ya vibanio (crush) kwa ajili ya kutolea chanjo ya
mifugo.
CHANJO NA KUOGESHA MIFUGO KAMA ZINAVYOFANYWA NA IDARA HII.
Afisa Mifugo kata ya Mwanga akifungua dawa aina ya Albadip kwa ajili ya kuiweka kwenye maji yatakayotumika kuogeshea mifugo. |
Hapa mtaalamu akimwagia dawa hiyo katika maji yatakayotumika kuogeshea mifugo. |
Huu ndio muonekano wa maji ya kuogeshea mifugo baada ya kumwagiwa dawa aina ya Albadip. |
Mifugo aina ya Ng'ombe na Mbuzi katika kata ya Mwanga ikisubiri kuogeshwa. |
Hivi ndivyo zoezi la kuingiza mifugo katika josho ilivyokuwa ikifanyika. |
PICHA NNE CHINI ZIKIMUONESHA MTAALAMU WA MIFUGO H/W MKALAMA, JOSEPH MICHAEL AKITOA HUDUMA YA CHANJO KATIKA KATA YA ILUNDA.
Idara ya Mifugo na uvuvi imefanikiwa kuingiza mapato ya
kiasi cha shilingi 31,871,500 mpaka sasa kutokana na chanjo ya Ng’ombe, Mbuzi
na Kondoo inayoendelea hivi sasa.
Zoezi hilo lipo kisheria chini ya Sheria ya Udhibiti wa
Magonjwa ya Mifugo namba 17 ya mwaka
2003 kifungu cha 28 na 62 ambayo inamtaka mfugaji yoyote kuipa kinga mifugo yake
na yoyote atakayevunja sheria hiyo adhabu yake ni faini isiyopungua shilingi
laki tatu au kifungo cha miezi sita gerezani au adhabu zote kwa pamoja.
Udhibiti wa magonjwa ya mifugo Mkalama hufanyika kila mwaka kwa njia mbili kuu kwa kuzingatia ratiba ya Wilaya ambazo ni Chanjo (Ng'ombe, Mbuzi, kondoo, Mbwa na Kuku) na Uogeshaji mifugo ambayo hufanyika kwa kuogesha mifugo kwenye majosho yaliyopo ndani ya Wilaya ili kudhibiti magonjwa mbalimbai yaenezwayo na Kupe kama vile Ndigana Kali (ECF), Ndigana baridi (Anaplasmosis), Mkojo damu (Babesiosis) na Majimoyo (Heart water).
Hii pia huambatana na udhibiti wa visumbufu vingine kama vile viroboto, Ndorobo na Chawa.
Njia ya pili ni udhibiti wa vidusi vya ndani (Internal Parasite) kama vile minyoo aina zote kwa njia ya chanjo (vaccination) au kunywesha dawa za minyoo (deworming).
Hii pia huambatana na udhibiti wa visumbufu vingine kama vile viroboto, Ndorobo na Chawa.
Njia ya pili ni udhibiti wa vidusi vya ndani (Internal Parasite) kama vile minyoo aina zote kwa njia ya chanjo (vaccination) au kunywesha dawa za minyoo (deworming).
Katika zoezi hilo, Ng’ombe wanapewa chanjo ya dawa aina
ya Lumpy Skin ambayo husaidia
kuondoa na kukomesha maradhi mbalimbali yanayosumbua mifugo hiyo.
Kwa upande wa mbuzi, dawa aina ya Ivomectin ndio iliyotumika katika chanjo hiyo ambayo ina nguvu na
uwezo maradufu ya dawa nyingine katika kukinga maradhi ya mifugo hiyo.
Idara ya Mifugo na uvuvi inapenda kutoa rai kwa wananchi
wote kwa ujumla kuhakikisha mifugo yao imepatiwa chanjo ili kuepukana na
magonjwa mbalimbali ambayo yamekuwa yakigharimu vifo vingi vya mifugo.
Aidha Idara ya Mifugo na Uvuvi imeanzisha zoezi la
uogeshaji wa mifugo katika kata zote ambapo zoezi hilo limeanzia kwenye kata ya
Mwanga.
Baada ya dawa nyingine kuonekana kutosaidia kuondoa
kabisa wadudu katika mifugo hiyo wakati wa zoezi la kuogesha , idara imeamua
kutumia dawa aina ya Albadip ambayo
imeonekana kumaliza kabisa tatizo la wadudu wanaosumbua mifugo hiyo.
IFUATAYO NDIO RATIBA YA UDHIBITI WA MAGONJWA YA KIFUGO KATIKA WILAYA YA MKALAMA KWA MWAKA 2016/2017.
IFUATAYO NDIO RATIBA YA UDHIBITI WA MAGONJWA YA KIFUGO KATIKA WILAYA YA MKALAMA KWA MWAKA 2016/2017.
Mhhhhh... Some amazing work my boy... Keep up the good work.
ReplyDelete