Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe: Jackson Masaka (mwenye trucsuit ya blue) akishiriki na watumishi na wananchi wa Wilaya hiyo katika zoezi la mchakamchaka. |
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama mhe: Jackson Masaka (kulia) akifanya mazoezi ya Viungo, katikati ni Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Bi. Rose Kibakaya. |
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama mhe: Jackson Masaka akionesha umahiri katika zoezi la kunyoosha misuli ya mkono kupitia kifaa maalum kwa zoezi hilo. |
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama mhe: Jackson Masaka akizindua mazoezi kwa kuruka kamba. |
Mwishoni mwa wiki iliyopita Wilaya ya Mkalama ilizindua
rasmi mazoezi ya mwili na viungo kwa watumishi wote wa Wilaya ikiwa ni
utekelezaji wa agizo la makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe:
Samia Suluhu Hassan.
Mazoezi hayo ambayo yalizinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya
Mkalama Mhe: Injinia Jackson Masaka yalijumuisha mbio fupi za mita 100 na ndefu
za mita 200, mpira wa miguu uliojumuisha taasisi mbalimbali za serikali, mpira
wa pete na mpira wa mikono.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mazoezi hayo Mhe:
Masaka alisema jambo hilo mbali na kuwa ni agizo kutoka kwa Makamu wa Rais, pia
ni muhimu sana kwa afya za watumishi na wananchi wote kwa ujumla kwa sababu
mazoezi hujenga mwili na kuuepusha na maradhi mbalimbali.
“Kupitia mazoezi hata matukio ya uhalifu na uvunjifu wa amani
yanapungua na kuisha kabisa kwa sababu mtu unakuwa umechoka sana hivyo hautakuwa
na muda wa kufikiria kufanya matukio hayo” Alisema Masaka.
Katika agizo lake Mhe: Samia aliwataka watumishi wote wa
serikali kushiriki katika mazoezi ya Mwili na Viungo kila jumamosi ya pili ya
Mwezi ili yaweze kuwasaidia kuondokana na maradhi mbalimbali ambayo yanaepukika
na kuongeza tija katika ufanyaji kazi wao wa kila siku.
No comments:
Post a Comment