Mbunge wa jimbo la Mkalama Mhe: Allan Kiula akizungumza machache wakati wa zoezi la kufunga mafunzo ya Jeshi la akiba ( Mgambo) lililofanyika katika kata ya Iguguno. |
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kushuhudia zoezi la ufungaji wa mafunzo ya jeshi la akiba (Mgambo) lililofanyika katika kata ya Iguguno. |
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama ambaye pia ni Mwenyekiti wa
kamati ya Ulinzi na Usalama Mhe: Jackson Masaka amewataka wazazi na walezi wote
Wilayani hapa kuhakikisha wanapeleka shuleni watoto wote waliochanguliwa kujiunga na idato cha
kwanza na wale ambao bado hawajaandikishwa kujiunga na elimu ya awali na msingi
waandikishwe kwa wakati kabla shule hazijafungua.
Mhe: Masaka ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya
jeshi la Akiba maarufu kama Mgambo yaliyoenda sambamba na sherehe za maadhimisho
ya miaka 55 ya uhuru wa Tanganyika katika
uwanja wa mpira wa Miguu wa Iguguno uliopo katika kata hiyo ambapo alisisitiza
kuwa serikali haitasita kuchukua hatua kwa mzazi au mlezi atakayepuuzia agizo
hilo kwa sababu dhamira ya dhati ya serikali iliyopo madarakani ni kuhakikisha
kila Mtanzania anapata Elimu na ndio maana imefuta malipo ya ada kutoka ngazi
ya awali mpaka kidato cha nne.
“Ningependa kuchukua fursa hii kuwapongeza sana vijana kwa
ujasiri na ukomavu waliouonesha katika kipindi chote cha mafunzo na
ninawahakikishia serikali itakuwa bega kwa bega na nyinyi pindi zitakapokuwa
zikitokea nafasi zinazohitaji ujuzi na mafunzo mliyoyapata” Alisisitiza Masaka.
Katika hatua nyingine, Mhe: Masaka aliwahimiza wananchi
kuhifadhi chakula walichopata wakati wa mavuno ya msimu uliopita wa kilimo kwa
sababu kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka ya hali ya hewa Tanzania,
Mikoa ya Dodoma na Singida itakuwa na mvua ya wastani kwa msimu wa mwaka
2016/2017 hivyo kuna hatari ya kukumbana na ukame kama wananchi hawatotunza
chakula cha akiba.
“Tulime mazao yatakayohimili ukame kama vile
mtama,uwele, viazi na mhogo lakini pia ili tujihakikishie kuwa na pesa ya
kununua chakula kutoka maeneo mengine tuweke vipaumbele kwenye mazao ya
biashara zaidi” Alimalizia Masaka.
No comments:
Post a Comment