PICHA 8: ZIARA YA MKUU WA MKOA WA SINGIDA MHE: MATHEW MTIGUMWE ALIPOENDA KUKAGUA UJENZI WA DARAJA LA SIBITI KATIKA KIJIJI CHA NYAHAA.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe: Injia Mathew Mtigumwe
amefanya ukaguzi wa daraja la Sibiti na kumtaka mkandarasi anayejenga daraja
hilo kuhakikisha linakamilika katika
muda uliopangwa.
Mhe: Mtigumwe ameyasema hayo Juzi alipoenda kufanya
ukaguzi ili kuona maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo ambapo alionekana
kuridhika na kasi ya ujenzi wake na kumtaka Mkandarasi huyo kuongeza kasi zaidi
ili likamilike kwa wakati.
“Daraja hili ni muhimu kwa Maendeleo ya wananchi wa
mikoa ya Simiyu na Singida pamoja na mikoa mingine ya kanda ya ziwa kutokana na
kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na wananchi na hivyo kuongeza kasi ya ukuaji
wa uchumi” Alisisitiza Mtigumwe.
Ujenzi wa daraja hilo ulisimama kwa kipindi cha miezi 30 kabla ya kuanza tena Mwezi Septemba
mwaka huu na unatarajiwa kukamilika mwezi disemba 2017 ambapo pia utajumuisha
ujenzi wa barabara za maungio zenye urefu wa kilomita 20.
No comments:
Post a Comment