Mratibu wa damu salama Wilayani Mkalama bi. Josephine Mwakanyaga akizungumza na vijana waliopo kwenye kambi ya mafunzo ya mgambo iliyopo kata ya Iguguno muda mfupi kabla ya vijana hao kuchangia damu. |
Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Dokta Deogratius Masini akizungumza na vijana waliopo kwenye kambi ya mafunzo ya mgambo katika kata ya Iguguno juu ya umuhimu wa kuchangia damu. |
Mmoja wa vijana wa kambi ya mafunzo ya mgambo akipimwa ili kujua wingi wa damu aliyonayo mwilini mwake kabla ya kuchangia. |
Idara ya Afya kupitia mpango wa damu salama Wilayani
hapa imeendelea kukusanya damu kutoka
kwa watu na vikundi vya watu mbalimbali ili kuhakikisha suala la ukosefu wa
damu katika vituo vya afya linakuwa historia.
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Dokta Deogratius
Masini aliongoza zoezi hilo lililofanyika jana katika kata ya Iguguno ambapo
vijana waliokuwa katika kambi ya mafunzo ya mgambo walijitolea kutoa damu.
Hata hivyo kwa mujibu wa mratibu wa Mpango wa damu
salama, bi. Josephine Mwakanyaga kiasi cha damu kilichokusanywa kwa mwezi kuanzia mwezi septemba mpaka novemba kipo
chini ya mahitaji halisi kwani kawaida mahitaji huwa ni uniti 28 kwa mwezi
lakini kiasi kilichokusanywa kwa miezi hiyo mitatu ni uniti 14, 14 na 8.
Pamoja na changamoto mbalimbali, Idara ya Afya Wilayani
Mkalama imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma
bora kadri inavyowezekana ikiwa ni pamoja na ofisi ya Mganga Mkuu kufanya
ukaguzi mara kwa mara katika vituo vya Afya ili kuhakikisha wananchi wanapata
huduma wanayostahili muda wote.
No comments:
Post a Comment