Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe: Jackson Masaka akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufika katika kata ya Ibaga mapema jana. |
Kaimu katibu tawala wa Wilaya ya Mkalama ndugu Pantaleo Molel akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya azungumze na wajumbe. |
Sehemu ya wajumbe wa baraza la ardhi la kata ya Mpambala wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Mkalama (hayupo pichani) mapema jana. |
Mkuu wa Shule ya Sekondari Chemchem akimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe: Jackson Masaka (katikati) orodha na aina ya vitabu vinavyopatikana katika maktaba ya shule hiyo. |
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe: Jackson Masaka akikagua vitabu vinavyopatikana katika maktaba ya shule ya sekondari Chemchem. |
Wanafunzi wa kidato cha nne wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Wilaya ya Mkalama (hayupo pichani) alipoingia darasani kwao kwa ajili ya kuwasalimu. |
Wanafunzi wa Shule ya sekondari Chemchem wakimuonesha Mkuu wa Wilaya Mkalama namna ya kutambua aina ya chakula kupitia majaribio ya somo la biolojia. |
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe: Jackson Masaka
amefanikiwa kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda mrefu baina ya ndugu
wawili wa familia moja, Mathayo Jonathan na Abel Jonathan wakazi wa kijiji cha Mpambala.
Katika uamuzi wake, Mhe: Masaka aliwataka ndugu hao
kuheshimu sheria na taratibu za nchi na waache kusumbua wajumbe wa baraza la
ardhi la kata na viongozi mbalimbali wa Wilaya na Mkoa kwa sababu tayari eneo
wanalogombania lilishatolewa maamuzi ya kumilikishwa kwa watu wengine.
“haiwezekani tena
shauri hilo kujadiliwa katika ngazi ya baraza la ardhi la kata kwa
sababu tayari eneo mnalogombania limeshatolewa hukumu na baraza la ardhi la
Wilaya na limeshahalishiwa umiliki wake kwa watu wengine” alisema Masaka.
Masaka alimuagiza katibu tawala wa Wilaya kuhakikisha
Abel Jonathan anamtafutia eneo jingine ndugu yake na suala hilo liwe limeisha
rasmi.
Wakazi hao walifikisha mgogoro wao katika baraza la
Ardhi la Kata ambalo lilisitisha usikilizaji wa suala hilo kutokana na eneo
wanalogombania kuwa na kesi nyingine ya Msingi katika baraza la Ardhi la Wilaya
ya Kiomboi.
Kesi hiyo ya baraza la Ardhi la Wilaya ilifunguliwa
na wananchi ambao walidai kununua eneo hilo kutoka kwa
Abel Jonathan baada ya Abel kupinga kuwauzia
eneo hilo.
Uamuzi wa baraza la Ardhi la Wilaya ndio ulioanzisha
mvutano baina ya ndugu hao wa familia moja kwani kabla ya kuuza eneo hilo, Abel
Jonathan alikuwa ameshamuuzia ndugu yake
Mathayo Jonathan ambaye anaishi Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora.
Kufuatia hukumu ya kuhalalisha umiliki wa eneo lile kwa
wale wananchi, Baraza la ardhi la Kata liliamuru Abel Jonathan amtafutie ndugu
yake eneo la kufidia kwa sababu halina mamlaka ya kupinga hukumu ya baraza la
Ardhi la Wilaya.
Mhe: Masaka pia alitumia fursa hiyo kukagua shule za
Msingi na Sekondari za Chemchem ambapo aliupongeza uongozi wa shule ya
sekondari ya Chemchem kwa kuwa na maktaba yenye vitabu vinavyoendana na mtaala
uliopo.
“Kuna shule ya binafsi niliwahi kuitembelea (jina
linahifadhiwa), vitabu vyake vyote ni “outdated” (muda wake wa kutumika
umeisha) na kila kitabu nachoulizia naambiwa hakipo” Aliongezea Masaka.
Alitoa Rai kwa wazazi na walezi wote Wilayani Mkalama
kuhakikisha ubora wa shule wanazopeleka watoto wao badala ya kujiridhisha na
ubora wa elimu inayotolewa kwa kuzingatia ukubwa wa ada za shule wanazolipa.
No comments:
Post a Comment