Tuesday, 11 October 2016

NDALICHAKO AZITUNUKU VYETI SHULE ZA MSINGI ZILIZOFANYA VIZURI MKALAMA.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Bw. Godfrey Sanga akizungumza na viongozi wa Idara ya Elimu  Msingi(waliokaa pembeni yake), Waratibu elimu kata na Wakuu wa shule za Msingi (hawapo pichani) katika kikao cha Idara ya Elimu Wilaya mapema leo mchana.

Afisa Elimu (Msingi) Wilaya ya Mkalama Bw. Chacha J. Kehogo akizungumza na waratibu Elimu kata na Wakuu wa shule waliofika kwenye kikao cha Idara ya Elimu Wilaya mapema leo mchana.



PICHA MBILI CHINI: Waratibu Elimu Kata na Wakuu wa shule za Msingi Wilaya ya Mkalama wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Bw. Godfrey Sanga (hayupo pichani) wakati wa kikao cha idara ya Elimu kilichofanyika mapema leo mchana.



Afisa Elimu Taaluma Bw. Mgoo Judson akisoma majina ya shule zilizofanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya darasa la saba mwaka huu.

PICHA 12 CHINI: Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Bw. Godfrey Sanga akikabidhi vyeti kwa wakuu wa shule za msingi zilizofanya vizuri kwenye matokeo ya Darasa la saba Mwaka 2016.














Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mntamba ambayo ndiyo iliyoongoza kwa ufaulu katika ngazi ya Wilaya  na kufanikiwa  kushika nafasi ya tatu ngazi ya Mkoa, Bi. Vones Kombe akipokea zawadi ya pesa taslimu kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Bw. Godfrey Sanga.

No comments:

Post a Comment

HALMASHAURI YA WILAYA MKALAMA