Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ofisini kwake Ikulu jijini Dar-salaam (picha kwa hisani ya mtandao) |
Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Mfuko wa Dunia wa Mazingira (GEF) na
Mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo (IFAD) inatarajia kuipa fursa ya
kipekee wilaya ya Mkalama baada ya kukamilika kwa utekelezaji wa mradi wa Kurejesha Ardhi
iliyoharibika na kuongeza uhakika na Usalama wa Chakula katika maeneo kame ya
Tanzania (LDFS).
Mradi
huo unaoendelea katika nchi 12 barani Afrika zilizopo kusini mwa jangwa la
Sahara unatarajiwa kutekelezwa katika vijiji vya Mpambala, Nyahaa, Lugongo na
Mkiko vilivyopo katika kata ya Mpambala.
Kupitia
mradi huo wananchi wa Mpambala watapata fursa ya kushiriki moja kwa moja kupitia
kamati za uwakilishi za vijiji zitakazoshirikisha jinsia zote ambapo zitakuwa
na kazi ya kupanga na kusimamia maliasili zilizopo kati ya vijiji kwa
kukubaliana katika upangaji na matumizi yanayozingatia usawa na kuandaa
miongozo.
Mradi huo unaotarajiwa kuanza
mapema mwezi ujao pia utaipa serikali
fursa ya kutambua teknolojia na maeneo yanayofaa kwa uvunaji wa mvua na maeneo ya vyanzo vya maji ambapo teknolojia
hiyo itasaidia kupunguza upotevu wa maji na kuongeza uzalishaji hasa kipindi
cha kiangazi kwa wananchi wa kata ya mpambala.
Wananchi wa vijiji vya kata ya
Mpambala pia watapatiwa mafunzo ya shamba darasa kuhusu kilimo hifadhi na mbinu
bora za kilimo rafiki kwa mazingira, uboreshaji na urutubishaji wa udongo,
mbinu za kilimo misitu, kilimo cha makinga maji, kilimo cha mzunguko na usimamizi
shirikishi wa kudhibiti wadudu na magonjwa ya mazao.
Mafunzo hayo yataenda sambamba
na kuwasaidia wakulima hao upatikanaji wa mbinu bora za kilimo na pembejeo katika mashamba darasa yatakayoanzishwa.
Mbali na Mkalama wilaya
nyingine zinazotekelezwa mradi huu hapa nchini ni Kondoa (Dodoma), Nzega
(Tabora), Magu (Mwanza) na Micheweni (Kaskazini Pemba).
No comments:
Post a Comment