“RUDI
MKALAMA, KUMENOGA!” Hiyo
ndio kauli inayoweza kutumika hivi sasa baada ya Wilaya ya Mkalama kufanikiwa
kushika nafasi ya kwanza kwa Halmashauri za Mkoa wa Singida kwenye maonesho ya
22 ya sikukuu ya wakulima na Wafugaji (NANENANE) yaliyohitimishwa leo hii na Naibu Waziri wa
Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Anthony Mavunde.
Ushindi huo unatokana na Wilaya hiyo kujidhatiti
kikamilifu katika sekta za Kilimo na Mifugo ambapo waliweza kuonesha kwa vitendo
kwa kuotesha mimea mbalimbali inayolimwa Wilayani Mkalama kupitia mashamba yao
yaliyopo hapa kwenye viwanja vya Nzuguni.
Mbali na mimea hiyo iliyostawi vizuri, Mkalama pia
wameweza kuonesha ustadi wa kufuga samaki na kuku ambapo wataalam wa mifugo na
uvuvi waliweza kuonesha namna bora kabisa ya kufuga kuku wa kienyeji na aina
mbalimbali za samaki kupitia bwawa lililopo nyuma ya banda lao la Maonesho.
Katika hali inayoonesha kujipanga zaidi kwa Uongozi wa
Wilaya ya Mkalama katika maonesho yajayo, Wilaya hiyo imeshatengeneza mabanda
ya kufugia Ng’ombe na Mbuzi hivyo kwa wageni watakaotembelea banda hilo kwenye
maonesho ya mwaka 2019 watapata fursa ya
kujifunza namna bora ya kufuga ng’ombe na mbuzi.
Mkalama
Guntooooooo!
No comments:
Post a Comment