Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Injinia Mathew Mtigumwe
jana alifanya ziara katika Wilaya za Mkalama na Iramba ikiwa ni ziara yake ya
kwanza tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo Machi 18 mwaka huu.
Mbali na kutumia
ziara hiyo kujitambulisha kwa watendaji mbalimbali wa wilaya hizo, Mtigumwe alitumia fursa hiyo kusisitiza
watendaji hao kufanya kazi kwa bidii ili kuendana na kasi ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania mheshimiwa John Pombe Magufuli ambapo aliwataka
kuhakikisha wanafanya kazi mara mbili au tatu ya walivyokuwa wakifanya kipindi
hicho.
“Kama tunalipwa mishahara kutoka kwenye kodi za wananchi,
hatuna budi kuhakikisha tunamaliza kero zote ambazo zinawakabili ili waweze
kufanya kazi kwa nguvu na kuongeza kipato” Alisema Mtigumwe.
Alisema watendaji wote wa serikali ni lazima watimize
wajibu wao kikamilifu na kama kuna kikao cha kisheria kwa ajili ya kujadili shughuli
za maendeleo ni lazima kikae bila
kungoja posho.
“Nimeagiza ndani ya miezi miwili idara zote za
mashauri ya walimu (TSD), zikae vikao na kusikiliza mashauri yote
yanayowahusu walimu” Aliongeza Mtigumwe.
Akisisitiza juu ya hilo Mtigumwe alisema kama kuna mtu wa
TSD ambaye hayupo tayari kukaa kwenye vikao hivyo mpaka apate posho aandike
jina lake kwa mkuu wa Wilaya ili atafutwe mtu ambaye yupo tayari kusikiliza na
kutatua kero za walimu.
“Hata madiwani pia, kama mnatakiwa kukaa vikao vya
kisheria msisubiri posho, kaeni alafu pesa ikikusanywa mtalipwa. Nchi haiwezi
kwenda kwa kusubiri posho muda wote na naomba posho zote ambazo si za kisheria
ila tulikuwa tukilipana baada ya mapato ya halmashauri kuwa makubwa zisitishwe
rasmi” Aliongeza.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Injinia Mathew Mtigumwe akisaini vitabu vya wageni katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkalama mara baada ya kuwasili jana. |
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Injinia Mathew Mtigumwe akizungumza na Watendaji na Watumishi wa Wilaya ya Mkalama jana. |
Baadhi ya Watumishi na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mheshimiwa Injinia Mathew Mtigumwe wakati akizungumza nao jana. |
|
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Injinia Mathew Mtigumwe akisaini vitabu vya wageni katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Iramba mara baada ya kuwasili jana. |
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Injinia Mathew Mtigumwe akisalimiana na wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Iramba mara baada ya kuwasili Wilayani hapo. |
Watendaji na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Injinia Mathew Mtigumwe (hayupo pichani) |
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Injinia Mathew Mtigumwe akipokea taarifa za awali kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Iramba, mheshimiwa Christopher Ngubiagai. ILI KUFAHAMU KWA UNDANI HISTORIA YA WILAYA YA MKALAMA, SHUGHULI ZAKE NA IDADI YA WATU WAKE KAMA ILIVYOSOMWA NA MKUU WA WILAYA HIYO MHESHIMIWA CHRISTOPHER NGUBIAGAI MBELE YA MKUU WA MKOA WA SINGIDA, bonyeza hapa UNAFAHAMU KUWA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA ALIMPA MKUU WA MKOA WA SINGIDA MHESHIMIWA INJINIA MATHEW MTIGUMWE JINA LA KINYIRAMBA ALIPOTEMBELEA WILAYANI HAPA JANA? bonyeza hapa. |
No comments:
Post a Comment