Thursday, 23 November 2017

KINACHOFANYWA NA TASAF MKALAMA

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ni moja ya nyenzo kuu ambazo serikali imezitumia katika kuhakikisha inainua maisha ya Watanzania  wa tabaka la chini ambapo lengo kuu huwa ni kuinua hali ya maisha ya watu hao angalau yafike katika tabaka la kati na wale wanaotumia vizuri fursa hii adimu hufika mpaka tabaka la juu.

Mara baada ya kuanza kufanikiwa kwa lengo mama la mfuko ambalo ni kutoa ruzuku isiyorejeshwa kwa walengwa, Mfuko ulianza kuangazia miundombinu mbalimbali inayowazunguka walengwa ambapo ulikusudia kupunguza au kuondoa changamoto zozote ambazo zitawafanya walengwa kushindwa kuzalisha kutokana na ruzuku wanazopewa.

Wilaya ya  Mkalama ni moja kati ya Maeneo ambayo mfuko umedhamiria  kuondoa kero mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili walengwa ambapo mchakato huu ulianza kwa kufanya tathmini ya changamoto zilizoibuliwa na kupewa kipaumbele na jamii husika.

Katika kijiji cha Senene , Mfuko unaendelea na ujenzi wa bwawa kubwa la maji na Uanzishwaji  wa Vitalu vya miti miradi ambayo ina thamani ya shilingi 19,985,500.00 huku miradi kama hiyo ikiwa imeanzishwa katika vijiji  vingine (gharama kwenye mabano) kama vile  Lukomo (28,165,000.00), Iguguno (63,735,000.00), Kidigida (19,529,500.00), Kidarafa (14,098,500.00), Mwanga (43,456,500.00), Nkalakala (22,168,500.00),  Msiu (26,028,500.00), Ipuli (25,762,500.00), Kinankamba (13,522,500.00), Mng’anda (8,733,500.00), Maziliga (12,907,000.00), Yulansoni (23,249,500.00), Kinyangiri (23,962,500.00), Ishenga (25,413,500.00), Singa (36,822,500.00), Iambi (19,047,500.00), Ilunda (34,018,000.00), Mbigigi (22,975,500.00), Dominic (18,881,500.00), Nkinto   (32,493,500.00), Makulo (15,081,500.00), Msingi (20,283,500.00), Ndurumo    (10,497,500.00) na Kijiji cha Kidii ambacho kinajengewa miradi kama hiyo kwa gharama ya Shilingi 19,631,500.00.

Eneo jingine ambalo limemulikwa na Mfuko huo Wilayani Mkalama ni Uondoaji  wa Makorongo katika vijiji  vya Milade utakaogharimu  jumla ya shilingi 27,977,000.00, Malaja (30,662,000.00), Marera (18,155,500.00), Miganga (30,038,000.00 na ujenzi wa bwawa) na  kijiji cha Nkungi mradi wenye thamani ya shilingi 29,040,000.00 ikiwa ni pamoja uanzishwaji wa Vitalu vya miti.

Mbali na miradi hiyo Mfuko umeangazia sekta ya barabara za kijamii ambapo Kijiji cha Kitumbili kimewezeshwa ujenzi wa barabara yenye urefu wa Km. 2.92 inayogharimu shilingi 24,412,000.00, Msisai yenye urefu wa Km 1.8  (16,445,000.00), Mgolombyo yenye urefu wa Km. 1.38 (33,822,000.00), Kinandili yenye urefu wa Km. 1.96 (17,744,000.00) na kijiji cha  Lyelembo kilichowezeshwa barabara yenye urefu wa Km. 4.16  inayogharimu shilingi 33,822,000.00.

Kufuatia tatizo la ukosefu wa maji ambalo huwa linayakumba maeneo mbalimbali katika Wilaya ya Mkalama, Mfuko umewezesha uchimbwaji wa visima katika vijiji mbalimbali huku gharama hizo zikijumuisha pia uanzishwaji wa Vitalu vya Miti kwa ajili ya kusaidia kutunza vyanzo hivyo vya maji ambapo kijiji cha Tumuli kimewezeshwa ukarabati wa visima vitatu vyenye thamani ya shilingi 16,848,500.00, Kijiji cha Mkunguru Visima vitano vyenye thamani ya shilingi 11,531,000.00, Kijiji cha Ikungu visima vitatu vyenye thamani ya Shilingi 18,622,500.00, Kijiji cha Mgimba Visima nane vyenye thamani ya shilingi 9,254,500.00 na Kijiji cha Mntamba kilichowezeshwa visima vinne vyenye thamani ya shilingi 20,834,500.00.

Jumla ya fedha ambazo serikali ya Tanzania kwa ushirikiano Mkubwa na Benki ya Dunia imeweza kuzitumia katika miradi hiyo Wilayani Mkalama ni shilingi 962,757,500.00

Pamoja na Serikali kutumia fedha nyingi kiasi hicho katika miradi ya wananchi bado changamoto kubwa imekuwa ni utunzaji wa miradi hiyo ambapo baadhi ya wananchi huwa wanaihujumu na kuwakosesha wengi huduma za msingi hivyo katika kuunga mkono jitihada zote hizi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano Wilayani Mkalama ni vizuri wananchi wote wahahakikishe miradi hii inatunzwa wakati wote ili iweze kuwa na manufaa kwa kizazi kilichopo na vijavyo.

No comments:

Post a Comment

HALMASHAURI YA WILAYA MKALAMA