Wednesday, 13 September 2017

Kuwasaidia 'Wakoma' ni jukumu letu sote-Masaka

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mhe. Mhandisi Jackson Masaka akimvalisha kofia kijana Daudi Daudi ambaye ana albinism wakati wa kugawa chakula na vitu mbalimbali kwa wahanga wa ugonjwa wa ukoma na watu wenye albinism katika kijiji cha Nkungi mapema jana.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mhe. Mhandisi Jackson Masaka akimpa vifaa mbalimbali vitakavyomsaidia mtoto Eliza ambaye ana albinism wakati wa kugawa chakula na vitu mbalimbali kwa wahanga wa ugonjwa wa Ukoma  na watu wenye albinism katika kijiji cha Nkungi mapema jana.

Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Daktari Deogratius Masini akimvalisha miwani ya jua kijana Daudi Daudi muda mfupi baada ya kukabidhiwa vifaa vyake. 

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mhe. Mhandisi Jackson Masaka akikagua misaada iliyotolewa na wadau mbalimbali muda mfupi kabla  ya kugawa chakula na vitu mbalimbali kwa wahanga wa ugonjwa wa ukoma  na watu wenye albinism katika kijiji cha Nkungi mapema jana.

Mkuu  wa Wilaya ya Mkalama, Mhe. Mhandisi Jackson Masaka(Mwenye suti Kulia) akikabidhi msaada wa nguo kwa wahanga wa ugonjwa wa Ukoma katika kijiji cha Nkungi mapema jana. 

Mkuu  wa Wilaya ya Mkalama, Mhe. Mhandisi Jackson Masaka (mwenye suti katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wahanga wa ugonjwa wa Ukoma katika kijiji cha Nkungi.

Diwani wa Kata ya Ilunda Mhe. Mohamedi Imbele akiwa na baadhi ya wahanga wa ugonjwa wa Ukoma maarufu kama 'wakoma' katika kijiji cha Nkungi mapema jana.


Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Mhandisi Jackson Masaka jana alitoa msaada wa chakula na mavazi kwa wahanga wa ugonjwa wa ukoma maarufu kama ‘wakoma’ wanaoishi katika kijiji cha Iambi Wilayani Mkalama.

Msaada huo umetokana na jitihada za dhati za Mhe. Masaka za kutafuta wadau mbalimbali wa kuwasaidia wahanga hao  na unajumuisha magunia 18 ya mahindi na viroba vitatu vya nguo ambazo hazijachakaa.

“Shukrani zangu za dhati ziende kwa kanisa la EAGT, kanisa la Maranatha,kanisa la KKKT wanzelya lililopo hapa Nkungi  na watu binafsi ambao wametoa na wanaendelea kutoa  michango mbalimbali kwa ajili ya wahanga hawa” Alisema Mhe. Masaka.

Naye Mwenyekiti wa shirika lisilo la serikali linalowasimamia wahanga hao (CHADEREREKO) bw. Martin Nakomolwa  amemshukuru Mhe. Masaka kwa jitihada zake za dhati za kuwasaidia wahanga hao na kuongeza kuwa hakuna Mkuu wa Wilaya ambaye amewahi kusimamia kikamilifu jambo hilo zaidi yake.

“Wote hapa ni mashahidi kuwa wamepita wengi katika Wilaya hii lakini hakuna aliyewahi kuguswa na suala la wakoma kwa kweli Mungu aendelee kukudumisha katika Wilaya yetu” Aliongeza Nakomolwa.

Akimkaribisha Mkuu wa Wilaya, Diwani wa kata ya Ilunda Mhe. Mohamedi Imbele amesema kuwa ni vyema misaada hiyo ikatumiwa na walengwa ili kuweza kutimiza haja ya wote waliojitolea kuwasaidia wahanga hao.

“Lakini mimi pia ntakuwa mchoyo wa fadhila kama sitamshukuru Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Mkalama kwa kazi nzuri anayoifanya katika Wilaya yetu hasa kupigania haki za wanyonge jambo ambalo ndio hasa muelekeo wa serikali ya awamu hii” Alimalizia Mhe. Imbele.

Wakati huo huo, Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Mhandisi Jackson Masaka alitumia nafasi hiyo kugawa vifaa mbalimbali kwa watu wawili wenye albinism ambapo jumla ya kofia za kujikinga na jua nne, Mafuta maalum ya ngozi, miwani pea nne iligawiwa kwa watu hao.


Ili kumuona na kumsikia Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Mhandisi Jackson Masaka wakati akizungumza jana tafadhali  bonyeza hapaNo comments:

Post a Comment

HALMASHAURI YA WILAYA MKALAMA