Wednesday 7 February 2018

Ni marufuku kuchukua chakula shuleni- Masaka

Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkalama Bi Elizabeth Rwegasira akimwaga mchanganyiko wa Saruji na Kokoto kama ishara ya Ujenzi wa Nyumba ya Watumishi wa Kituo cha Afya cha Knyambuli

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Mhandisi Jackson Masaka akichanganya kokoto na saruji kwenye ujenzi wa Maabara ya Kituo cha Afya cha Kinyambuli ikiwa ni  sehemu ya  Maadhimisho ya Miaka 41 ya Chama cha Mapinduzi.

Mgeni Rasmi wamaadhimisho ya 41 ya kuzaliwa Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Mhandisi Jackson Masaka akijenga ukuta wa Chumba cha Wodi ya Wazazi ya Kituo cha Afya cha Kinyambuli ikiwa ni  sehemu ya  Maadhimisho hayo yaliyofanyika katika kijiji cha Kinyambuli leo.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Mhandisi Jackson Masaka akishindilia kokoto kwenye sakafu ya Nyumba ya watumishi wa Kituo cha Afya cha Kinyambuli ikiwa ni sehemu ya  Maadhimisho ya Miaka 41 ya Chama cha Mapinduzi.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Mhandisi Jackson Masaka akimkabidhi mmoja wa wazee wa kijiji cha Kinyambuli Mche wa Sabuni ikiwa ni sehemu ya  Maadhimisho ya Miaka 41 ya Chama cha Mapinduzi.




‘’Una Chakula kitamu kiasi gani nyumbani kwako mpaka mtoto wako asile na wenzake shuleni?’’

Hilo ni swali lililoulizwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Mhandisi Jackson Masaka alipoalikwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Mgeni Rasmi kwenye maadhimisho ya miaka 41 tangu kuzaliwa kwa chama hicho yaliyofanyika Kiwilaya katika Kijiji cha Kinyambuli.

Mhe. Masaka amewasisitiza wazazi na walezi wote kuwa Msimamo wa Wilaya ya Mkalama ni watoto wote wapate chakula shuleni kwa sababu Wilaya imedhamiria kupandisha kiwango cha Ufaulu hivyo ni lazima wanafunzi watumie muda mwingi kufundishwa na kusoma shuleni.

‘’Mhe. Rais hajakataza michango shuleni  isipokuwa ameondoa jukumu la kukusanya michango hiyo kwa walimu ili wajikite zaidi kutoa taaluma na si vinginevyo hivyo ninaagiza kuanzia sasa ni marufuku kwa mzazi au mlezi kwenda shuleni kudai kurejeshewa chakula alichokuwa ametoa kwa ajili ya mtoto wake”. Amesisitiza Mhe. Masaka.

Katika hatua nyingine Mhe. Masaka amesema  kuwa Serikali ya Awamu ya tano imefanya mambo mengi sana na ya Msingi Wilayani Mkalama ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa daraja la kisasa la Sibiti linalotarajiwa kukamilishwa hivi karibuni, Ujenzi wa madarasa, bwalo na mabweni katika shule ya Sekondari Iguguno uliyoifanya Shule hiyo kuwa ya kwanza kuwa na wanafunzi wa kidato cha tano na Uboreshaji wa Kituo bora na cha Kisasa cha Kinyambuli.

“Rai yangu kwenu wananchi wa Kinyambuli naomba muwe wazalendo juu ya mradi huu na msiukwamishe kwa namna yoyote kwa sababu pamoja na kuwanufaisha wakazi wote wa Mkalama, nyie mnabaki kuwa wanufaikaji wakuu kutokana na mradi huu kujengwa katika kijiji chenu” Amesisitiza Mhe. Masaka.

No comments:

Post a Comment

HALMASHAURI YA WILAYA MKALAMA