Sunday 1 May 2016

MKALAMA WAPAMBA MEI MOSI



























Sherehe za Mei mosi zimefanyika leo Mkoani Singida ambapo zilibeba kauli mbiu isemayo “dhana ya mabadiliko ilenge kuinua hali za wafanyakazi”.

Sherehe hizo ambazo hufanyika kila mwaka zilianza kwa maandamano ya wafanyakazi wa sekta mbalimbali yaliyoanzia katika uwanja wa Shirikisho la vyama vya wafanyazi (TUCTA) mpaka katika uwanja wa Namfua ambapo ndipo maadhimisho hayo yalipokuwa yakifanyika.

Wafanyakazi kutoka Wilaya za Itigi, Iramba, Manyoni, Ikungi na Mkalama zilishiriki katika maadhimisho hayo ambapo kila Wilaya ilikuwa na bango maalum lenye ujumbe mahsusi kwa viongozi wa juu wa serikali, mgeni rasmi na wafanyakazi wenzao kwa ujumla.

Katika sherehe hizo wafanyakazi hodari kutoka vyama mbali mbali vya wafanyakazi ikiwemo TUICO, TALGWU, CWT, TUGHE n.k  walipewa zawadi mbalimbal  ambapo zawadi ya juu kabisa ilitolewa na shirika la Umeme nchini (TANESCO) mkoani Singida ambao waliwazawadia watumishi wao televisheni bapa aina ya Samsung  zenye thamani ya shilingi milioni moja na laki mbili.

Wafanyakazi hao ni wale ambao wameteuliwa na Idara na Vitengo vyao wanavyovifanyia kazi katika ofisi zao.

No comments:

Post a Comment

HALMASHAURI YA WILAYA MKALAMA