Friday, 4 August 2017

Bidhaa za Mkalama ni lazima zilitangaze Taifa pia- Mhe. Mndeme

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mndeme akitoa somo kwa wajasiriamali wa Wilaya ya Mkalama juu ya namna ya kulitangaza Taifa kupitia bidhaa zao alipotembelea banda la Wilaya hiyo jioni hii.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mndeme akipewa somo na mtaalam wa masuala ya chakula tiba kutoka Wilaya ya Mkalama Daktari Gerlard Minja alipotembelea banda la Wilaya ya Mkalama jioni hii.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mndeme akipata Maelezo kutoka kwa mhudumu katika kitengo cha Upimaji wa Virusi vya Ukimwi na Ushauri Nasaha (hayupo pichani) alipotembelea banda la Wilaya ya Mkalama jioni hii.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mndeme akiangalia namna ya ufugaji wa kuku alipotembelea katika banda la Wilaya ya Mkalama jioni hii.


Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mndeme leo ametembelea banda la NaneNane la Wilaya ya Mkalama ambapo amevutiwa na kazi nzuri zinazofanywa na wajasiriamali, Wakulima na wafugaji wa Wilaya ya Mkalama na kuwataka waanze kupanua soko la nje.

“Mnaweza kudhani mnachofanya ni kitu kidogo lakini nawahakikishia Mkalama mnafanya kazi kubwa sana na jitihada zenu zinaonekana hasa kupitia haya ninayoyaona hapa kwa hiyo nawashauri muanze kuangalia soko la nje la bidhaa zenu”  Aliongeza Mhe.  Mndeme.

Mhe. Mndeme amewashauri wajasiriamali na wakulima wa Wilaya ya Mkalama kuzitambulisha bidhaa zao kwa misingi ya kitaifa zaidi ili wanapouza bidhaa zao hata nje ya nchi waweze kuitangaza na Tanzania kwa ujumla.

“Mfano huu mvinyo mzuri mnapouuza kwa mgeni itakuwa ngumu kujua umetokea nchi gani kwa sababu huenda hata katika nchi nyingine kuna sehemu inaitwa Mkalama au Singida hivyo ni vyema mmalizie kabisa kwa kutambulisha kuwa bidhaa hii inatokea Tanzania” Alisisitiza Mhe. Mndeme.


Mhe. Mndeme alimalizia kwa kuupongeza uongozi mzima wa Wilaya ya Mkalama, Wakulima, wafugaji na wananchi wote kwa ujumla kwa kuwa wabunifu na kuitangaza vyema Wilaya yao katika Nyanja za Kilimo, Mifugo na Ujasiriamali.

Kumsikiliza na kumuona Mhe.  Christina Mndeme alipotembelea banda la Mkalama jioni hii Bofya hapa.

No comments:

Post a Comment

HALMASHAURI YA WILAYA MKALAMA