Monday 7 August 2017

Kitunguu cha Mkalama ni cha Kimataifa- Nchimbi

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Daktari Rehema Nchimbi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufika katika banda la Wilaya ya Mkalama.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Daktari Rehema Nchimbi  akitoa maagizo na Maelekezo kwa Viongozi na watendaji mbalimbali wa halmashauri ya Wilaya ya Mkalama alipofika katika banda la Wilaya hiyo leo jioni.

PICHA TATU CHINI: MKUU WA MKOA WA SINGIDA MHE. DAKTARI REHEMA NCHIMBI AKITOA MAELEKEZO MARA BAADA YA KUKAGUA BWAWA LA KUFUGIA SAMAKI LILILOJENGWA NYUMA YA BANDA YA MAONESHO LA WILAYA YA MKALAMA




Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Daktari Rehema Nchimbi akioneshwa kuku waliofugwa na vikundi vya wafugaji wa halmashauri ya Wilaya ya Mkalama.


PICHA NANE CHINI: MKUU WA MKOA WA SINGIDA MHE. DAKTARI REHEMA NCHIMBI AKIKABIDHIWA ZAWADI MBALIMBALI NA VIKUNDI VYA WAKULIMA NA WAJASIRIAMALI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA MARA BAADA YA KUMALIZA ZIARA YAKE KATIKA BANDA LA MAONESHO LA WILAYA HIYO.











Mapema leo jioni  Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Daktari Rehema Nchimbi ametembelea banda la halmashauri ya Wilaya ya Mkalama ambapo ametoa maagizo mbalimbali kwa Mkurugenzi, Mwenyekiti wa Halmashauri na Afisa Kilimo wa Wilaya kuhakikisha maonesho yanayokuja ya Nanenane yanakuwa na tija kubwa hata kwa mwananchi wa Mkalama ambaye hajabahatika kufika katika Maonesho ya kikanda.

Mhe. Nchimbi amesema kuwa Kuanzia sasa Wilaya ya Mkalama itenge eneo kubwa ambalo litawekwa vipando ambavyo vitakuwa hapo kwa kipindi cha Mwaka mzima ili wananchi ambao hawatopata fursa ya kushiriki katika maonesho ya kikanda na kitaifa watumie nafasi hiyo kwenda kujifunza kilimo bora na cha kisasa.

“Ninaposema mwaka mzima namaanisha katika maeneo hayo mfanye utaratibu wa kuchimba visima kwa sababu mvua haipatikani mwaka mzima na hapo wananchi kutoka sehemu mbalimbali watafika na kupata elimu tena vipando hivyo mnaweza kuviita ‘NaneNane Mkalama Mubashara’ mkimaanisha wananchi watakuja kujifunza  moja kwa moja kutoka shambani” Amesisitiza  Mhe. Nchimbi.

Mhe. Nchimbi amesema kuwa kitendo hicho kitawafanya wananchi wote wa Mkalama waone umuhimu wa sikukuu ya NaneNane kwa sababu pamoja na kutofika katika maonesho ya kikanda na kitaifa bado watakuwa wamepata elimu inayofanana na wale waliohudhuria maonesho hayo kikanda na kitaifa.

“Ikifika Mwezi Septemba nitafuatilia hili ili nijue kama utekelezaji wake umeanza” Ameongeza Mhe. Nchimbi.

Mhe. Nchimbi pia ameagiza  halmashauri ya Wilaya ya Mkalama ihakikishe imetangaza bidhaa zake kila inapotimia robo mwaka na bidhaa hizo zisiishie kutangazwa katika redio za mikoani tu bali ununuliwe muda katika vituo vya Televisheni pia.

“Kupitia vipindi hivyo tangazeni kila kinachozalishwa Mkalama vikiwemo vitunguu, asali, nyanya na kwa kufanya hivyo mtakuwa mmetangaza soko la Mkalama sio tu kitaifa bali kimataifa” Amesisitiza Mhe. Nchimbi.

Mhe. Nchimbi amesifia Vitunguu vinavyozalishwa katika Wilaya ya Mkalama ambapo amesema vina ubora wa kimataifa na hata sokoni ndio vitunguu vinavyopewa kipaumbele kuliko vitunguu vinavyozalishwa katika maeneo mengine.


“Kuna baba mmoja ni mstaafu wa jeshi alilima vitunguu katika Mkoa wa Morogoro tena vitunguu vizuri tu lakini alipovipeleka sokoni alikataliwa na kuambiwa vitunguu pekee vinavyonunuliwa hapo ni vile vinavyotoka Mkoani Singida kwa hiyo tangazeni sana bidhaa zenu kwa sababu zina thamani kubwa sana sokoni” Alimalizia Mhe. Nchimbi.

Ili uweze kumuona Mhe. Nchimbi akitoa maagizo hayo bofya hapa

No comments:

Post a Comment

HALMASHAURI YA WILAYA MKALAMA