Tuesday 14 February 2017

MKALAMA WAMEFANYA UZINDUZI WA MAZOEZI YA VIUNGO

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe: Jackson Masaka (mwenye trucsuit ya blue)  akishiriki na watumishi na wananchi wa Wilaya hiyo katika zoezi la mchakamchaka.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama mhe: Jackson Masaka (kulia) akifanya mazoezi ya Viungo, katikati ni Afisa Elimu Vifaa na Takwimu  Bi. Rose Kibakaya.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama mhe: Jackson Masaka akionesha umahiri katika zoezi la kunyoosha misuli ya mkono kupitia kifaa maalum kwa zoezi hilo. 
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama mhe: Jackson Masaka akizindua mazoezi kwa kuruka kamba.



Mkuu wa Wilaya ya Mkalama mhe: Jackson Masaka na kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya hiyo, Injinia Ramadhani Mohamed (waliovaa trucksuit za blue) wakiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa michezo mbalimbali iliyofanyika siku hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama mhe: Jackson Masaka akizungumza maneno machache wakati wa uzinduzi wa mazoezi hayo. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mkalama Injinia Ramadhani Mohamed na kushoto ni kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Bi. Josephine Makanyaga.


Mwishoni mwa wiki iliyopita Wilaya ya Mkalama ilizindua rasmi mazoezi ya mwili na viungo kwa watumishi wote wa Wilaya ikiwa ni utekelezaji wa agizo la makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe: Samia Suluhu Hassan.

Mazoezi hayo ambayo yalizinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe: Injinia Jackson Masaka yalijumuisha mbio fupi za mita 100 na ndefu za mita 200, mpira wa miguu uliojumuisha taasisi mbalimbali za serikali, mpira wa pete na mpira wa mikono.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mazoezi hayo Mhe: Masaka alisema jambo hilo mbali na kuwa ni agizo kutoka kwa Makamu wa Rais, pia ni muhimu sana kwa afya za watumishi na wananchi wote kwa ujumla kwa sababu mazoezi hujenga mwili na kuuepusha na maradhi mbalimbali.

“Kupitia mazoezi hata matukio ya uhalifu na uvunjifu wa amani yanapungua na kuisha kabisa kwa sababu mtu unakuwa umechoka sana hivyo hautakuwa na muda wa kufikiria kufanya matukio hayo” Alisema Masaka.

Katika agizo lake Mhe: Samia aliwataka watumishi wote wa serikali kushiriki katika mazoezi ya Mwili na Viungo kila jumamosi ya pili ya Mwezi ili yaweze kuwasaidia kuondokana na maradhi mbalimbali ambayo yanaepukika na kuongeza tija katika ufanyaji kazi wao wa kila siku.
          

No comments:

Post a Comment

HALMASHAURI YA WILAYA MKALAMA