Thursday, 10 November 2016

NIMERIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA DARAJA-MTIGUMWE

PICHA 8: ZIARA YA MKUU WA MKOA WA SINGIDA MHE: MATHEW MTIGUMWE ALIPOENDA KUKAGUA UJENZI WA DARAJA LA SIBITI KATIKA KIJIJI CHA NYAHAA.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe: Injia Mathew Mtigumwe amefanya ukaguzi wa daraja la Sibiti na kumtaka mkandarasi anayejenga daraja hilo  kuhakikisha linakamilika katika muda uliopangwa.

Mhe: Mtigumwe ameyasema hayo Juzi alipoenda kufanya ukaguzi ili kuona maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo ambapo alionekana kuridhika na kasi ya ujenzi wake na kumtaka Mkandarasi huyo kuongeza kasi zaidi ili likamilike kwa wakati.

“Daraja hili ni muhimu kwa Maendeleo ya wananchi wa mikoa ya Simiyu na Singida pamoja na mikoa mingine ya kanda ya ziwa kutokana na kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na wananchi na hivyo kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi” Alisisitiza Mtigumwe.


Ujenzi wa daraja hilo ulisimama kwa kipindi cha  miezi 30 kabla ya kuanza tena Mwezi Septemba mwaka huu na unatarajiwa kukamilika mwezi disemba 2017 ambapo pia utajumuisha ujenzi wa barabara za maungio zenye urefu wa kilomita 20.

No comments:

Post a Comment

HALMASHAURI YA WILAYA MKALAMA