Saturday, 26 November 2016

DAMU SALAMA YASHIKA KASI MKALAMA

Mratibu wa damu salama Wilayani Mkalama bi. Josephine Mwakanyaga akizungumza na vijana waliopo kwenye kambi ya  mafunzo ya mgambo iliyopo kata ya Iguguno  muda mfupi kabla ya vijana hao kuchangia damu.

Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Dokta Deogratius  Masini akizungumza na vijana waliopo kwenye kambi ya mafunzo ya mgambo katika kata ya Iguguno juu ya umuhimu wa kuchangia damu.

Mmoja wa vijana wa kambi ya mafunzo ya mgambo akipimwa ili kujua wingi wa damu aliyonayo mwilini mwake kabla ya kuchangia.

Mratibu wa damu salama Wilayani Mkalama bi. Josephine Mwakanyaga akimuelekeza mmoja wa vijana waliojitolea kuchangia damu namna ya kujaza kadi yake.

PICHA 6 CHINI: JINSI ZOEZI LA UCHANGIAJI DAMU LILIVYOFANYIKA.
Idara ya Afya kupitia mpango wa damu salama Wilayani hapa  imeendelea kukusanya damu kutoka kwa watu na vikundi vya watu mbalimbali ili kuhakikisha suala la ukosefu wa damu katika vituo vya afya linakuwa historia.

Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Dokta Deogratius Masini aliongoza zoezi hilo lililofanyika jana katika kata ya Iguguno ambapo vijana waliokuwa katika kambi ya mafunzo ya mgambo walijitolea kutoa damu.

Hata hivyo kwa mujibu wa mratibu wa Mpango wa damu salama, bi. Josephine Mwakanyaga kiasi cha damu kilichokusanywa kwa mwezi  kuanzia mwezi septemba mpaka novemba kipo chini ya mahitaji halisi kwani kawaida mahitaji huwa ni uniti 28 kwa mwezi lakini kiasi kilichokusanywa kwa miezi hiyo mitatu ni uniti 14, 14 na 8.

Mwakanyaga amebainisha changamoto kubwa inayoukabili mpango huo ni ukosefu wa jokofu na chumba cha kuhifanyia damu hiyo wilayani hapa hali inayolazimu damu inayokusanywa Wilayani hapa kupelekwa kuhifadhiwa katika hospitali ya Mkoa wa Singida.

Pamoja na changamoto mbalimbali, Idara ya Afya Wilayani Mkalama imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora kadri inavyowezekana ikiwa ni pamoja na ofisi ya Mganga Mkuu kufanya ukaguzi mara kwa mara katika vituo vya Afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma wanayostahili muda wote.No comments:

Post a Comment

HALMASHAURI YA WILAYA MKALAMA