Monday 3 October 2016

ZIARA YA KIGWANGALA WILAYANI MKALAMA

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia na Watoto Mhe: Hamisi Kigwangala (mwenye fulana ya njano)  akiwasili katika halmashauri ya Wilaya ya Mkalama huku akilakiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe: Jackson Masaka (katikati) na kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Chacha Kehogo (kushoto).

Picha mbili chini akisalimiana na baadhi ya watumishi




Hapa akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya.

Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya dokta Deogratius Masini akisoma taarifa fupi ya Idara ya Afya mbele ya Mhe: Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia na watoto.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe: Jackson Masaka akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mhe: Naibu waziri (Kulia).

Muuguzi wa zamu katika zahanati ya Nduguti, Bi. Josephine Mwakanyaga akitoa maelekezo juu ya namna zanahati hiyo inavyofanya kazi mbele ya Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto, Mhe: Hamisi Kigwangala.


Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia na watoto, Mhe: Hamisi Kigwangala akitoa sifa na pongezi kwa muuguzi wa zamu wa zahanati ya Nduguti, Bi. Josephine Mwakanyaga (katikati) baada ya kumpa maelekezo mazuri na yaliyojitosheleza kuhusiana na zahanati hiyo.


Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia na watoto, Mhe: Hamisi Kigwangala akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Chacha Kehogo (kulia) wakati wa ziara yake Wilayani hapa.


Hapa akikagua dawa na vifaa tiba vinavyopatikana katika kituo cha Afya  Kinyangiri.

Hapa akizungumza na wananchi wa kata ya Iguguno wakati akihitimisha ziara yake Wilayani hapa.




 Naibu Waziri wa Afya, Mendeleo ya jamii, jinsia na watoto, Mhe: Hamisi Kingwangala amefanya ziara Wilayani hapa wikiendi hii ambapo mbali  na kutembelea na kukagua kazi mbalimbali zinazofanywa na Idara ya afya, ametoa maagizo.


Katika ziara hiyo, Kigwangala alianza kwa kutembelea Zahanati ya Nduguti ambapo alitoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mkalama kuhakikisha anamaliza ujenzi wa Jengo la Kituo cha Afya cha  Wilaya ndani ya Miezi sita.

“Kama mtaendelea kusubiri pesa za bajeti ili mkamilishe jengo hili mtakuwa mnajichelewesha wenyewe kwa sababu kwa hatua lililofikia mna uwezo wa kulimalizia kwa kutumia vyanzo vya ndani” Aliongeza Kigwangala.

Katika hatua nyingine, Mhe: Kigwangala alimsifu mhudumu wa Zahanati hiyo, Josephine Mwakanyaga ambaye ndiye aliyekuwa akimpa maelezo mbalimbali yanayohusu zahanati hiyo kwa uwezo mkubwa alionao katika uchambuzi wa dawa na vifaa tiba.

“Huyu ni mhudumu mwenye uwezo mkubwa sana na anayejua kitu anachofanya” Alisema Kigwangala.

Ziara ya Mhe: Kigwangala ilihitimishwa katika Zahanati ya Iguguno ambapo alimsifu Mbunge wa jimbo la Mkalama Mhe: Allan Kiula na timu yote ya Halmashauri ya Wilaya kwa hatua waliyolifikisha jengo jipya linalotarajiwa kuwa kituo cha afya katika eneo hilo.

“Nawapongeza sana na ninawaahidi kuwaunga mkono kwa kuhakikisha taratibu za usajili wa kituo hiki zinafanyika haraka sana ili lianze kutumika mara moja mara baada ya kukamilika” Alimalizia Kigwangala.

Aidha katika kuunga mkono jitihada za Mhe: Kiula, Kigwangala aliahidi kuchangia shilingi milioni moja ili kukamilisha ujenzi wa Jengo hilo.









No comments:

Post a Comment

HALMASHAURI YA WILAYA MKALAMA