Monday 23 May 2016

WASHINDI KOMBE LA MEI MOSI WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO

Zawadi za washindi wa kombe la Mei mosi zikiwa meza kuu kabla ya kukabidhiwa kwa washindi

Wawakilishi wa timu zilizofanikiwa kushika nafasi tatu za juu katika fainali za kombe la Mei Mosi wakimsikiliza Mgeni rasmi kabla ya kukabidhiwa zawadi zao.

Mratibu wa Mashindano ya kombe la Mei mosi ambaye pia ni Afisa habari wa Wilaya ya Mkalama, Omary Mtamike (kushoto) akitoa taarifa fupi ya mashindano hayo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ili aweze kutoa hotuba na zawadi kwa washindi.

Washindi wa pili wa mashindano ya Kombe la Mei Mosi, timu ya Nduguti Stars wakionesha zawadi yao ya mpira  mara baada ya kukabidhiwa.

Afisa Tawala wa Wilaya ya Mkalama ambaye pia alikuwa mgeni rasmi wa hafla ya utoaji zawadi kwa washindi, akikabidhi zawadi ya kombe wa washindi wa kwanza wa mashindano ya kombe la Mei mosi, timu ya Watumishi.

Washindi wa kwanza wa kombe la Mei Mosi, timu ya Watumishi wakishangilia mara baada ya kukabidhiwa kombe lao na mpira.
Baada ya kufanikiwa kuchukua ubingwa wa kombe la Mei Mosi hatimaye timu ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama ilifanikiwa kukabidhiwa zawadi yao ya Kombe, Mpira na Pesa taslimu shilingi 50,000 kama zilivyoahidiwa na muandaaji wa mashindano hayo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe: Christopher Ngubiagai.

Zawadi hizo zilikabidhiwa mwishoni mwa wiki iliyopita katika hafla fupi iliyoandaliwa na Mkuu huyo wa Wilaya na kufanyika katika Ukumbi wa hoteli maarufu ya Wakawaka iliyopo Wilayani hapa.

Mbali na zawadi hizo kwa washindi wa kwanza, washindi wa pili ambao  walikuwa ni timu ya Nduguti Stars walifanikiwa kuchukua zawadi ya Mpira na pesa taslimu kiasi cha shilingi 30000 na timu ya Kisulwiga ambayo ilifanikiwa kutwaa nafasi ya tatu ilipewa mpira na pesa taslimu kiasi cha shilingi elfu 20.

Katika hotuba yake ambayo ilisomwa kwa niaba yake na Afisa Tawala wa Wilaya, ndugu Pantaleo Molel, Ngubiagai alisema ni vizuri waandaaji wa mashindano hayo wakaongeza idadi ya michezo katika mashindano yajayo ili kuongeza chachu Zaidi na idadi ya ushiriki.

“Ningependa kuwapongeza washindi wote watatu na washiriki wengine wote wa mashindano haya ya Mei mosi kwa sababu mashindano haya yamezidi kuimarisha Amani, mshikamano na upendo kwa wananchi wote wa Wilaya ya Mkalama, Alimalizia Pantaleo.

2 comments:

  1. Mkalama oyeee,thanx DC natimu nzima ya maandalizi.

    ReplyDelete
  2. Mkalama oyeee,thanx DC natimu nzima ya maandalizi.

    ReplyDelete

HALMASHAURI YA WILAYA MKALAMA