|
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Bravo Kizito Lyapembile akikagua mashamba ya Vitunguu muda mfupi kabla ya kumpokea Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe: Mathew Mtigumwe alipofanya ziara katika kata ya Gumanga jana. |
|
Afisa Kilimo wa Wilaya ya Mkalama Cuthbert Mwinuka (kulia) akitoa akitoa maelekezo juu ya namna ya kulimwa zao la nyanya kwa njia ya Umwagiliaji mbele ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Bravo Kizito Lyapembile. |
|
Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Cuthbert Mwinuka akionesha namna pump ya umwagiliaji mazao inavyofanya kazi. |
|
Hili ndio jengo la Kiwanda cha Kusindika Nyanya ambalo linatarajiwa kukamilika na kuanza kazi muda wowote kuanzia sasa. |
|
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe: Injinia Mathew Mtigumwe (wa pili kutoka kushoto) akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Mkalama mara baada ya kuwasili katika eneo la kiwanda cha kusindika Nyanya katika kata ya Gumanga. |
|
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe: Mathew Mtigumwe akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika eneo la kiwanda cha kusindika Nyanya kwenye Kata ya Gumanga. Aliyekaa kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe: Christopher Ngubiagai. |
PICHA SABA ZIFUATAZO ZINAMUONESHA AFISA KILIMO WA WILAYA YA MKALAMA, CUTHBERT MWINUKA AKITOA MAELEKEZO JUU YA NAMNA KIWANDA KITAKAVYOFANYA KAZI ZAKE MBELE YA MKUU WA MKOA WA SINGIDA NA UJUMBE WAKE.
|
Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Cuthbert Mwinuka ( kushoto) akitoa maelekezo juu ya kilimo cha zao la Kitunguu mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Singida na ujumbe kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. |
|
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe: Mathew Mtigumwe (katikati) akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe: Christopher Ngubiagai (nyuma yake) na ujumbe kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. |
|
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe: Mathew Mtigumwe na ujumbe wake wakimsikiliza Mkulima waliyemkuta shambani jana. |
|
Afisa Kilimo wa Wilaya ya Mkalama Cuthbert Mwinuka akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida na ujumbe wake uliofika katika mashamba ya Gumanga |
|
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe; Mathew Mtigumwe akizungumza na Vijana waliojikita kwenye kilimo katika kata ya Gumanga. |
|
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe: Mathew Mtigumwe(Kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe: Christopher Nguabiagai wakimsikiliza mmoja wa wajumbe wa kikundi cha wanawake wajasiriamali wakati akiwaelekeza namna ya kutengeneza tomato. |
|
Hili si ndoo ya Maji bali ni mtambo wa kutengeneza mvinyo kwa kutumia nyanya kama ulivyowasilishwa na kikundi cha Wanawake wajasiriamali katika Kata ya Gumanga. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe: Christopher Ngubiagai (Kushoto) akisaini kitabu cha wageni huku akishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe: Mathew Mtigumwe. |
|
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe: Mathew Mtigumwe akihutubia wananchi wa kata ya Gumanga katika ziara yake jana. |
|
Mara baada ya kumaliza hotuba yake, Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe: Mathew Mtigumwe alikabidhiwa zawadi na Kikundi cha wanawake wajasiriamali wa kata ya Gumanga kama inavyyonekana pichani. |
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Injinia Mathew Mtigumwe amesisitiza wakulima
kujiunga na vikundi vidogo na vikubwa
ili waweze kupatiwa Mikopo itakayowawezesha kuendeleza miradi yao kwa urahisi.
Mtigumwe ameyasema hayo alipofanya ziara katika Kiwanda cha
kusindika zao la nyanya kinachotarajiwa kuanza kufanya kazi muda wowote kuanzia sasa ambapo kitasaidia
wakulima wanaolima zao hilo katika kata ya Gumanga na maeneo ya karibu kupata
sehemu ya kuuza mazao yao.
“Kupitia kiwanda hiki sasa mtaweza kuzalisha nyanya kwa
wingi kwa sababu mmeshapata sehemu ya kuuza badala ya awali ambapo mlikuwa
mkiuza kwa hasara au kuyaacha yakiharibika shambani”. Alisema Mtigumwe.
Akisisitiza kuhusu suala hilo la kujiunga na vikundi
Meneja wa Shirika la viwanda vidogo (SIDO) mkoani Singida , Shoma Kibende
alisema shirika hilo lina uwezo wa kukopesha kila mwanachama aliyepo kwenye
kikundi kiasi cha shilingi laki tano hivyo alishauri wanakijiji wa kata ya Gumanga
wajiunge kwenye vikundi ili iwe rahisi kwao kukopesheka.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa wa Singida
alimmwagia sifa Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe: Christopher Ngubiagai na safu
yote ya watendaji wake kwa kazi nzuri ya kutekeleza maagizo yote wanayopewa
huku ikiongoza katika kila kampeni za kitaifa zinazotangazwa ikiwemo ya maabara
pamoja na madawati.
“ Kwa kweli Mkalama mnastahili sifa sana kwa sababu kila
kampeni ya kitaifa mmekuwa mkiongoza kwa Mkoa wote wa Singida na nimeambiwa
hata hili la madawati mbali na kuongoza mpaka hivi sasa, mtalimaliza rasmi
tarehe 15 mwezi huu, hongereni sana”,
Alisema Mtigumwe.
Aliongeza juu ya hilo kwa kuwashauri wakurugenzi na
wenyeviti wa halmashauri za wilaya nyingine za mkoa huo kufika katika Wilaya ya
Mkalama na kujifunza ni namna gani
wanaweza kutekeleza maagizo kwa mafanikio.
No comments:
Post a Comment