Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe: Christopher Ngubiagai akizungumza na ujumbe wa wahadzabe uliofika ofisini kwake mapema jana. |
Ujumbe wa jamii ya wahadzabe ukimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Mkalama (katikati) alipokuwa akizungumza nao jana. |
Mwenyekiti wa jamii ya wahadzabe Edward Mashimba (mwenye suti ya blue) akiwa na wawakilishi wengine wa jamii hiyo huku wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe: Christopher Ngubiagai. |
Kikao kilichofanywa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya na ofisi ya
Mkurugenzi wa halmshauri ya Wilaya ya Mkalama tarehe 20/05/2016 katika kata ya
Munguli kuhusiana na suala la jamii ya Wahadzabe kunyang’anywa maeneo yao
kimezaa matunda baada ya jamii hiyo kukubali kupimiwa maeneo yao ili waweze
kuyamiliki kisheria.
Ujumbe wa wawakilishi sita wa jamii hiyo uliofika katika
ofisi za Wilaya ya Mkalama na kukutana na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe: Christopher Ngubiagai,
umesema kuwa wahadzabe wameamua kufanyia kazi ushauri uliotolewa na Mkuu wa
Wilaya na kuungwa mkono na kaimu afisa ardhi wa Wilaya ya Mkalama Imikigwe
Mwanitu kuwa maeneo yote wanayomiliki yapimwe ili wawe na umiliki wa kisheria.
Ujumbe huo ulioongozwa na Mwenyekiti wa jamii ya Wahadzabe
waishio Wilaya ya Mkalama ndugu Edward Mashimba umemshukuru Mkuu wa Wilaya hiyo
kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha hawanyang’anywi haki yao ya kumiliki
maeneo ambayo wamekuwa wakiyamiliki kwa miaka mingi sasa.
Akizungumza wakati wa mazungumzo hayo ofisini kwake, Mhe: Ngubiagai
aliipongeza jamii yote ya wahadzabe kwa kukubali ushauri wake na kuchukua hatua
hiyo ya kukubali kupimiwa maeneo yao na kuahidi kuwasaidia kulinda rasilimali
hiyo.
“kwa sababu mkishapimiwa mtakuwa mkiyamiliki maeneo hayo
kisheria, ofisi yangu itahakikisha hakuna uvamizi wowote unaofanyika katika
maeneo yenu na yoyote atakayevamia basi sheria itafuata mkondo wake, Alisema
Ngubiagai.
Mwisho wa mazungmzo hayo mafupi, Mwenyekiti wa wahdazabe
alimuombea dua ya kihadzabe Mkuu huyo wa Wilaya iliyobeba ujumbe wa kumtakia
afya njema na ulinzi katika shughuli zake za kila siku za kuwahudumia wananchi.
Mbali na Mwenyekiti wa jamii ya wahadzabe, wajumbe wengine
walioambatana nae ni Charles Mtani, Mathayo Wilson, Marta Marko, Pendo Daniel
na Elineema Martini.
No comments:
Post a Comment