Zawadi za washindi wa kombe la Mei mosi zikiwa meza kuu kabla ya kukabidhiwa kwa washindi |
Wawakilishi wa timu zilizofanikiwa kushika nafasi tatu za juu katika fainali za kombe la Mei Mosi wakimsikiliza Mgeni rasmi kabla ya kukabidhiwa zawadi zao. |
Washindi wa pili wa mashindano ya Kombe la Mei Mosi, timu ya Nduguti Stars wakionesha zawadi yao ya mpira mara baada ya kukabidhiwa. |
Washindi wa kwanza wa kombe la Mei Mosi, timu ya Watumishi wakishangilia mara baada ya kukabidhiwa kombe lao na mpira. |
Baada ya kufanikiwa kuchukua ubingwa wa kombe la Mei Mosi hatimaye
timu ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama ilifanikiwa kukabidhiwa
zawadi yao ya Kombe, Mpira na Pesa taslimu shilingi 50,000 kama zilivyoahidiwa
na muandaaji wa mashindano hayo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe:
Christopher Ngubiagai.
Zawadi hizo zilikabidhiwa mwishoni mwa wiki iliyopita
katika hafla fupi iliyoandaliwa na Mkuu huyo wa Wilaya na kufanyika katika
Ukumbi wa hoteli maarufu ya Wakawaka iliyopo Wilayani hapa.
Mbali na zawadi hizo kwa washindi wa kwanza, washindi wa
pili ambao walikuwa ni timu ya Nduguti
Stars walifanikiwa kuchukua zawadi ya Mpira na pesa taslimu kiasi cha shilingi
30000 na timu ya Kisulwiga ambayo ilifanikiwa kutwaa nafasi ya tatu ilipewa
mpira na pesa taslimu kiasi cha shilingi elfu 20.
Katika hotuba yake ambayo ilisomwa kwa niaba yake na Afisa
Tawala wa Wilaya, ndugu Pantaleo Molel, Ngubiagai alisema ni vizuri waandaaji
wa mashindano hayo wakaongeza idadi ya michezo katika mashindano yajayo ili
kuongeza chachu Zaidi na idadi ya ushiriki.
“Ningependa kuwapongeza washindi wote watatu na washiriki
wengine wote wa mashindano haya ya Mei mosi kwa sababu mashindano haya yamezidi
kuimarisha Amani, mshikamano na upendo kwa wananchi wote wa Wilaya ya Mkalama,
Alimalizia Pantaleo.
Mkalama oyeee,thanx DC natimu nzima ya maandalizi.
ReplyDeleteMkalama oyeee,thanx DC natimu nzima ya maandalizi.
ReplyDelete