Wednesday, 14 December 2016

KILA MTOTO MKALAMA NI LAZIMA AENDE SHULE- MASAKA

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya hiyo, Mhe: Jackson Masaka akikagua gwaride wakati wa kufunga mafunzo ya jeshi la akiba (mgambo) yaliyofanyika katika kata ya Iguguno.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya hiyo, Mhe: Jackson Masaka akipokea salamu ya utii kutoka kwa kiongozi wa mafunzo ya Jeshi la akiba (Mgambo) wakati wa kufunga mafunzo ya jeshi hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya hiyo, Mhe: Jackson Masaka akipokea risala fupi aliyosomewa wakati wa kufunga mafunzo ya jeshi la akiba (mgambo) yaliyofanyika katika kata ya Iguguno.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya hiyo, Mhe: Jackson Masaka akikabidhiwa zawadi baada ya kufanikiwa kuwa mlengaji  pekee aliyefanikiwa kupiga eneo la moyo la adui wakati akizindua zoezi la ulengaji wa shabaha maarufu kama "range"

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya hiyo, Mhe: Jackson Masaka akinawa mikono mara baada ya kupanda mti wakati wa ufungaji wa mafunzo ya jeshi la akiba (mgambo) zoezi lililofanyika katika kata ya Iguguno.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya hiyo, Mhe: Jackson Masaka akihutubia wananchi waliojitokeza kushuhudia zoezi la ufungaji wa mafunzo ya jeshi la akiba (mgambo) katika kata ya Iguguno.

Mbunge wa jimbo la Mkalama Mhe: Allan Kiula akizungumza machache wakati wa zoezi la kufunga mafunzo ya Jeshi la akiba ( Mgambo) lililofanyika katika kata ya Iguguno.


Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mkalama, Ndugu Chacha J. Kehogo (kulia) akifuatilia kwa makini maonesho ya jeshi la akiba (mgambo) wakati wa ufungaji wa mafunzo ya jeshi hilo yaliyofanyika katika kata ya Iguguno.

PICHA 12 CHINI:  MAONESHO MBALIMBALI YA MAFUNZO WALIYOYAFANYA WANAJESHI WA JESHI LA AKIBA (MGAMBO) MBELE YA MGENI RASMI, WAALIKWA WENGINE NA WANANCHI WALIOJITKEZA KUSHUHUDIA.

Sehemu ya wananchi waliojitokeza kushuhudia zoezi la ufungaji wa mafunzo ya jeshi la akiba (Mgambo) lililofanyika katika kata ya Iguguno.Mkuu wa Wilaya ya Mkalama ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama Mhe: Jackson Masaka amewataka wazazi na walezi wote Wilayani hapa kuhakikisha wanapeleka shuleni watoto  wote waliochanguliwa kujiunga na idato cha kwanza na wale ambao bado hawajaandikishwa kujiunga na elimu ya awali na msingi waandikishwe kwa wakati kabla shule hazijafungua.

Mhe: Masaka ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya jeshi la Akiba maarufu kama Mgambo yaliyoenda sambamba na sherehe za maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru wa Tanganyika  katika uwanja wa mpira wa Miguu wa Iguguno uliopo katika kata hiyo ambapo alisisitiza kuwa serikali haitasita kuchukua hatua kwa mzazi au mlezi atakayepuuzia agizo hilo kwa sababu dhamira ya dhati ya serikali iliyopo madarakani ni kuhakikisha kila Mtanzania anapata Elimu na ndio maana imefuta malipo ya ada kutoka ngazi ya awali mpaka kidato cha nne.

“Ningependa kuchukua fursa hii kuwapongeza sana vijana kwa ujasiri na ukomavu waliouonesha katika kipindi chote cha mafunzo na ninawahakikishia serikali itakuwa bega kwa bega na nyinyi pindi zitakapokuwa zikitokea nafasi zinazohitaji ujuzi na mafunzo mliyoyapata” Alisisitiza Masaka.

Katika hatua nyingine, Mhe: Masaka aliwahimiza wananchi kuhifadhi chakula walichopata wakati wa mavuno ya msimu uliopita wa kilimo kwa sababu kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka ya hali ya hewa Tanzania, Mikoa ya Dodoma na Singida itakuwa na mvua ya wastani kwa msimu wa mwaka 2016/2017 hivyo kuna hatari ya kukumbana na ukame kama wananchi hawatotunza chakula cha akiba.

“Tulime mazao yatakayohimili ukame kama vile mtama,uwele, viazi na mhogo lakini pia ili tujihakikishie kuwa na pesa ya kununua chakula kutoka maeneo mengine tuweke vipaumbele kwenye mazao ya biashara zaidi” Alimalizia Masaka.No comments:

Post a Comment

HALMASHAURI YA WILAYA MKALAMA