Friday, 22 April 2016

VIKAO VYA KISHERIA VISISUBIRI POSHO-MKUU WA MKOA SINGIDA

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Injinia Mathew Mtigumwe jana alifanya ziara katika Wilaya za Mkalama na Iramba ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo Machi 18 mwaka huu.

Mbali na kutumia  ziara hiyo kujitambulisha kwa watendaji mbalimbali wa wilaya hizo,  Mtigumwe alitumia fursa hiyo kusisitiza watendaji hao kufanya kazi kwa bidii ili kuendana na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa John Pombe Magufuli ambapo aliwataka kuhakikisha wanafanya kazi mara mbili au tatu ya walivyokuwa wakifanya kipindi hicho.

“Kama tunalipwa mishahara kutoka kwenye kodi za wananchi, hatuna budi kuhakikisha tunamaliza kero zote ambazo zinawakabili ili waweze kufanya kazi kwa nguvu na kuongeza kipato” Alisema Mtigumwe.

Alisema watendaji wote wa serikali ni lazima watimize wajibu wao kikamilifu na kama kuna kikao cha kisheria kwa ajili ya kujadili shughuli za maendeleo ni lazima kikae  bila kungoja posho.

“Nimeagiza ndani ya miezi miwili  idara zote za  mashauri ya walimu (TSD), zikae vikao na kusikiliza mashauri yote yanayowahusu  walimu” Aliongeza Mtigumwe.

Akisisitiza juu ya hilo Mtigumwe alisema kama kuna mtu wa TSD ambaye hayupo tayari kukaa kwenye vikao hivyo mpaka apate posho aandike jina lake kwa mkuu wa Wilaya ili atafutwe mtu ambaye yupo tayari kusikiliza na kutatua kero za walimu.


“Hata madiwani pia, kama mnatakiwa kukaa vikao vya kisheria msisubiri posho, kaeni alafu pesa ikikusanywa mtalipwa. Nchi haiwezi kwenda kwa kusubiri posho muda wote na naomba posho zote ambazo si za kisheria ila tulikuwa tukilipana baada ya mapato ya halmashauri kuwa makubwa zisitishwe rasmi” Aliongeza.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Injinia Mathew Mtigumwe akisalimiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mkalama  Ndugu Bravo K. Lyapembile mara baada ya kuwasili Wilayani hapo  jana, nyuma yake (aliyevaa kaunda suti) ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mheshimiwa Christopher Ngubiagai.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Injinia Mathew Mtigumwe akisaini vitabu vya wageni katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkalama mara baada ya kuwasili jana.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Injinia Mathew Mtigumwe akizungumza na Watendaji na Watumishi wa Wilaya ya Mkalama jana. 

Baadhi ya Watumishi na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mheshimiwa Injinia Mathew Mtigumwe wakati akizungumza nao jana.

Baadhi ya Watumishi na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mheshimiwa Injinia Mathew Mtigumwe wakati akizungumza nao jana.


Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Injinia Mathew Mtigumwe akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na Watendaji wa Wilaya ya Mkalama. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mheshimiwa James Nkwega. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mheshimiwa Christopher Ngubiagai akifuatiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Ndugu Bravo K. Lyapembile na wa mwisho ni Katibu tawala wa Wilaya ya Mkalama Ndugu Benjamin Mwombeki. Waliosimama ni waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama.


Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Injinia Mathew Mtigumwe akisaini vitabu vya wageni katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Iramba mara baada ya kuwasili jana.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Injinia Mathew Mtigumwe akisalimiana na wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Iramba mara baada ya kuwasili Wilayani hapo.
Watendaji na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Injinia Mathew Mtigumwe (hayupo pichani)

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Injinia Mathew Mtigumwe akipokea taarifa za awali kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Iramba, mheshimiwa Christopher Ngubiagai.

ILI KUFAHAMU KWA UNDANI HISTORIA YA WILAYA YA MKALAMA, SHUGHULI ZAKE NA IDADI YA WATU WAKE KAMA ILIVYOSOMWA NA MKUU WA WILAYA HIYO MHESHIMIWA CHRISTOPHER NGUBIAGAI MBELE YA MKUU WA MKOA WA SINGIDA,  bonyeza hapa

UNAFAHAMU KUWA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA  ALIMPA MKUU WA MKOA WA SINGIDA MHESHIMIWA  INJINIA MATHEW MTIGUMWE JINA LA KINYIRAMBA ALIPOTEMBELEA WILAYANI HAPA JANA?  bonyeza hapa.


No comments:

Post a Comment

HALMASHAURI YA WILAYA MKALAMA