Saturday 14 June 2014

KILIMO CHA NYANYA GUMANGA

Gumanga ni kijiji kilichopo katika wilaya ya mkalama. Wakazi wa kijiji hiki wamekuwa wakijihusisha na kilimo cha nyaya kama zao lao la biashara kwa ajili ya kujipatia kipato. Ukifika katika kijiji hiki utashangaa kuona akina mama wakiwa na ndoo, vikapu na vichanja vilivyojaa nyanya hii ni kuonyesha kuwa zao hili limekuwa likiwaokoa sana wamama katika kujipatia fedha za kujikimu katika familia zao.

Kilimo cha nyanya Gumanga.
Kilimo hiki cha mazao ya bustani kinawafaidisha sana wakazi hawa kwani wanaweza kulima misimu mitatu  kwa mwaka na gharama ya kulima ni ndogo. Wastani wa mapato kwa ekeri ni Tshs 8,540,000/=, kila msimu wanaweza kupata faida ya Tshs 4,000,000/= (milioni nne) .Hivyo kwa mwaka huwa na kipato cha wastani wa Tshs. 12,000,000/=. Kwa ujumla pamoja na shughuli zao za kila siku za kilimo cha mazao mengine kama Uwele, mtama, mihogo, vitunguu na alizeti, ambayo huwaingizia kipato. Wakazi hawa wana uhakika wa kupata mapato ambayo hayana tofauti na kima cha chini cha mshahara wa mtumishi wa Serikali.


Wanaishukuru Serikali ya awamu ya nne na Viongozi wake wote kwa kuwajali  wajasiriamali wadogo Vijijini kwa kuwaboreshea  maisha, pia wanaishukuru Halmashauri yao ya Wilaya ya Mkalama kwa kuwawezesha kupata pembejeo za kilimo na zana za kumwagilia  zenye thamani ya tshs 940,000/=ili waweze kuzalisha kwa njia za kisasa.

No comments:

Post a Comment

HALMASHAURI YA WILAYA MKALAMA