Friday, 23 May 2014

UJIO WA KATIBU MKUU WA CCM


Kesho tarehe 24 May 2014 wananchi wa Mkalama wanajipanga kumpokea katibu mkuu wa CCM Taifa Bwana Abrahman Kinana anayetarajiwa kufika wilayani Mkalama kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM inayotoa sura kamili ya maendeleo ya wananchi.
Katika ziara hiyo Mh. Kinana atakagua miradi mbalimbali ikiwepo Daraja la Sibiti linalojengwa na Serikali ya CCM litakalounganisha Wilaya ya Mkalama na Mkoa kwa ujumla na Wilaya ya Meatu ya Mkoa wa Shinyanga, Pia atakagua shughuli za kimaendeleo za wananchi katika vijiji vya Gumanga na Nduguti na hatimaye atashiriki katika shughuli ya ujenzi wa Maabara ya Shule ya Sekondari Gunda iliyoko kijiji cha Nkungi.
Aidha ujio huu utatoa fursa kwa wananchi wa mkalama kutoa kero zao walizonazo.
Ziara hii ni miongoni mwa ziara muhimu zinazofanywa na chama cha CCM katika mikoa yote Tanzania yenye lengo la kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za kujiletea maendeleo pale wanapoweza na sio kusubiri mkono wa Serikali.

No comments:

Post a Comment

HALMASHAURI YA WILAYA MKALAMA