Saturday 25 June 2016

HONGERENI SANA MKALAMA-JAFO

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe: Selemani Jafo akisalimiana na Mkuu wa gereza la Singa mara baada ya kuwasili mapema leo asubuhi, Aliyesimama katikati ni Mbunge wa Jimbo la Mkalama, Mhe: Allan Kiula.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe: Selemani Jafo, akielekea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa ajili ya kusaini kitabu cha wageni.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe: Selemani Jafo akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya.

PICHA SITA ZIFUATAZO ZINAMUONESHA INJINIA WA WILAYA, RAMADHANI MOHAMEDI AKITOA MAELEZO MBALIMBALI JUU YA UJENZI WA JENGO LA HALMASHAURI MBELE YA MHE: NAIBU WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS, TAMISEMI, SELEMANI JAFO.









Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe: Selemani Jafo, akimpa maelekezo kaimu Afisa Ardhi wa Wilaya, Imikigwe Mwanitu (Mwenye fulana ya bluu) alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya Wilaya mapema leo.

Mkandarasi kutoka kampuni ya Mzinga akitoa maelekezo juu ya namna ukamilishaji wa ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya Wilaya utakavyofanyika.


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe: Selemani Jafo akimpa maelekezo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Bravo Kizito Lyapembile (katikati) wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa Jengo la halmashauri ya Wilaya mapema leo asubuhi.

Kaimu Afisa Elimu wa Wilaya ya Mkalama, Nasibu Pangahela akisoma taarifa fupi ya idara ya Elimu mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe: Selemani Jafo kabla ya zoezi la kukabidhi madawati.

Haya ndio madawati aliyokabidhiwa Mheshimiwa Waziri leo na Mbunge wa jimbo la Mkalama, Mhe: Allan Kiula.

Mbunge wa jimbo la Mkalama Mhe: Allan Kiula akimkabidhi madawati 100 yaliyotokana na mfuko wa jimbo, Mhe: Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Selemai Jafo.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe: Selemani Jafo akikabidhi madawati kwa mmoja waWAkuu wa Shule za sekondari mara baada ya kukabidhiwa na Mhe: Mbunge mapema leo asubuhi.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe: Selemani Jafo akimpongeza mtengenezaji mkuu wa madawati hayo Lameck mara baada ya kukabidhi kwa wakuu wa Shule.


Sehemu ya Wananchi wa Wilaya ya Mkalama waliojitokeza kumsikiliza Naibu waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe: Selemani Jafo katika eneo la Stendi mapema leo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Bravo Kizito Lyapembile akisoma taarifa fupi ya Wilaya mbele ya Mhe: Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo (hayupo pichani) 

Mbunge wa jimbo la Mkalama Mhe: Allan Kiula akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Mkalama muda mfupi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mh: Selemani Jafo.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe: Selemani Jafo akihutubia wananchi wa Wilaya ya Mkalama waliojitokeza kumsikiliza mapema leo asubuhi.


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kisarawe leo amefanya ziara fupi katika halmashauri ya Wilaya ya Mkalama ambapo amewataka watendaji wa serikali kufanya kazi zao kwa weledi na kuhakikisha ofisi zao zinamaliza kero zote za wananchi.

Huku akizungumza mbele ya umati wa watu waliojitokeza kumsikiliza mara baada ya kukabidhi madawati, Mhe: Jafo amesema ni jambo la kushangaza kwa halmashauri kuendelea kuwa na madai ya watumishi kutopandishwa madaraja wakati ofisi ya Utumishi ipo.

“Kuanzia sasa, akitokea mtu yoyote kulalamika kutopandishwa daraja, Afisa Utumishi tutakuondoa kwenye nafasi yako” Alisisitiza Jafo.

Kwa upande wa Idara ya Maendeleo ya jamii, Mhe: Jafo amemtaka Afisa Maendeleo ya jamii kupitia ofisi yake, ahakikishe wametoa elimu ya kutosha kwa vikundi vya vijana na wanawake juu ya namna watakavyotumia mkopo wa Milioni 50 alizoahidi Mhe: Rais ambazo zitatoka muda wowote kuanzia sasa.

“Afisa Maendeleo ya jamii ndio injini ya kuchochea maendeleo ya vijana na jamii inayokuzunguka hapa Wilayani lakini cha kushangaza wengi wenu mmekuwa mkionekana zaidi pindi pesa za Tasaf na Mradi wa Ukimwi zinapotoka na huenda hata hii jamii iliyopo mbele yangu hapa haikutambui, Naomba mbadilike” Aliongeza Jafo.

Kabla ya kuzungumza na wananchi hao Mhe: Jafo alikabidhiwa madawati 100 yaliyotolewa na Mfuko wa Mbunge wa jimbo hilo ambapo aliwapongeza viongozi, watendaji na wananchi wote wa Mkalama kwa kumaliza kabisa tatizo la madawati Wilayani hapa.

“ Madawati ndio kipimo kikubwa kwa wakurugenzi na wakuu wa Wilaya wote nchini hivyo ukiona hujakamilisha suala hili ujue nafasi hiyo haikutoshi tena lakini nawapongeza Mkalama mmeshavuka mtego huo hivyo mpo salama” Ameongeza Jafo.

Mara baada ya kufika Wilayani hapa mapema leo, Mhe: Jafo alifanya ziara ya kukagua Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na pamoja na jengo la halmashauri ya Wilaya ambalo limefikia hatua ya Lenta mpaka hivi sasa na awamu ya kwanza inatarajiwa kukamilika muda wowote kuanzia hivi sasa.

Baada ya kuona namna ujenzi wa jengo hilo unavyoendelea kwa kasi, Mhe: Jafo alimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Bravo Kizito Lyapembile kwa kazi nzuri ya kujenga jengo lenye ubora tena kwa kutumia mkandarasi wa ndani.

“Niliwahi kwenda Halmashauri ya Mwanga nikakuta jengo la serikali limeshatoa nyufa zaidi ya 20 tena kabla hata halijaanza kutumika, Lakini ukiuliza Mkandarasi anasema “Consultant” hajasema chochote ndio maana naye ameacha hali iwe hivyo, Lakini Mkalama mmemtumia Mkandarasi wa Wilaya kusimama kama “consultant” tena kwa mshahara huo huo anaolipwa na serikali, Hongereni sana” Alipongeza Jafo.

Kufuatia suala hilo Mhe: Jafo Aliagiza Wilaya nyingine zifike Mkalama kujifunza namna ya kusimamia kazi za serikali bila kufuja fedha za umma ambazo zinatokana na kodi za wananchi.

Kabla ya kuondoka katika eneo hilo, Mhe: Jafo aliagiza majengo yote ya serikali  nchini kuhakikisha yanakuwa na hati miliki ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima siku za usoni.



No comments:

Post a Comment

HALMASHAURI YA WILAYA MKALAMA