Sherehe za Mei mosi zimefanyika leo Mkoani Singida ambapo
zilibeba kauli mbiu isemayo “dhana ya mabadiliko ilenge kuinua hali za
wafanyakazi”.
Sherehe hizo ambazo hufanyika kila mwaka zilianza kwa
maandamano ya wafanyakazi wa sekta mbalimbali yaliyoanzia katika uwanja wa
Shirikisho la vyama vya wafanyazi (TUCTA) mpaka katika uwanja wa Namfua ambapo
ndipo maadhimisho hayo yalipokuwa yakifanyika.
Wafanyakazi kutoka Wilaya za Itigi, Iramba, Manyoni, Ikungi
na Mkalama zilishiriki katika maadhimisho hayo ambapo kila Wilaya ilikuwa na
bango maalum lenye ujumbe mahsusi kwa viongozi wa juu wa serikali, mgeni rasmi
na wafanyakazi wenzao kwa ujumla.
Katika sherehe hizo wafanyakazi hodari kutoka vyama mbali
mbali vya wafanyakazi ikiwemo TUICO, TALGWU, CWT, TUGHE n.k walipewa zawadi mbalimbal ambapo zawadi ya juu kabisa ilitolewa na
shirika la Umeme nchini (TANESCO) mkoani Singida ambao waliwazawadia watumishi
wao televisheni bapa aina ya Samsung zenye thamani ya shilingi milioni moja na laki
mbili.
Wafanyakazi hao ni wale ambao wameteuliwa na Idara na
Vitengo vyao wanavyovifanyia kazi katika ofisi zao.
No comments:
Post a Comment