|
Katibu Mkuu wa CCM - Taifa akiongea na wananchi wa Gumanga |
Wananchi wa Mkalama leo walikuwa kwenye shamrashamra za
kumpokea Mh. Abrahman Kinana Ambaye ni katibu mkuu wa CCM Taifa aliyefika
katika Wilaya ya Mkalama kwa lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Akitokea Iramba Mh. Kinana alipokelewa katika wilaya ya Mkalama mnamo saa mbili
asubuhi (8:00 am) ambapo mara baada ya kufika alikwenda moja kwa moja kukagua
Daraja la Sibiti linalojengwa ambalo litafungua mawasiliano na wilaya ya Meatu.
Wakiwa katika furaha kubwa wananchi wa Mkalama walicheza kwa
bidii na katika kuonyesha furaha yao walipiga na kucheza ngoma ya Kinyiramba
ijulikanayo kama MBUTU ngoma ambayo hupigwa kwenye matukio maalum. Pia kwaya na
vikundi mbalimbali vya filimbi viliwafurahisha watu waliojitokeza kuhudhuria
mkutano.
|
Mwananchi akikatika. |
|
Wananchi wa Mkalama wakipiga
na kucheza ngoma ya MBUTU |
|
Mzee akipuliza mbutu. |
Baada ya hapo alihutubia wananchi wa kijiji cha Gumanga,
Nduguti, Nkungi na Iguguno ambapo aliwataka kutokubweteka na watu wanaojidai
kutetea maslahi ya nchi kwa kudai serikali tatu na badala yake wamesahau
kuwaletea wananchi maendeleo. Pamoja na hayo Mheshimiwa Kinana alivitaja vijiji
vitakavyopata umeme ikiwa ni juhudi za CCM kuwaletea maendeleo wananchi, vijiji
hivyo ni Kinyangiri, Ishenga, Nduguti, Gumanga, Kisuluiga, Nkalakala, Mwando,
Iambi, Ilunda n.k katika kusisitiza jambo hilo aliwataka wananchi kujiandaa
kulipia tsh 27,000 ili waingiziwe umeme katika hatua ya awali ambayo ni bei
nafuu sana. Pia alivitaja vijiji vya Nkinto, Matongo, Munguli, Dominiki n.k
ambavyo vitapata mawasiliano ya simu. Mheshimiwa kinana pia aliwaeleza wananchi
wa Nkungi kuwa barabara inayotoka Singida kupitia Ilongero, Mtinko Singa,
Nkungi, Mpaka Nduguti ipo kwenye mpango wa kutengenezwa kwa kiwango cha lami na
barabara ya Iguguno, Nduguti, Ibaga kupitia daraja la sibiti itakuwa ya lami
jambo ambalo litaleta maendeleo kwa wananchi wa Mkalama. Pia zaidi ya Tsh 2
bilioni zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za Wilaya, Halmashauri na
Nyumba za watumishi.
Nape Nnauye naye alizidi kuwaomba wananchi kuendelea
kukiamini chama cha mapinduzi kwa kuwa ndio chama pekee kitakachowaletea
maendeleo.
|
Nape Nnauye |
|
Mh. Mwigulu Nchemba |
Mheshimiwa Kinana aliambatana na Nape Nnauye ambaye ni Katibu
wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba Naibu katibu Mkuu
na Mbunge wa Iramba Magharibi, Salome Mwambu Mb. wa jimbo la Iramba Mashariki
(Mkalama), Mather Mlata Mbunge Viti Maalum na M/kiti CCM Mkoa Mh. Msindai. Pia
Mkuu wa Mkoa wa Singida Kone na Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Edward Ole Lenga nao
walikuwepo kwenye ziara hii. Pamoja na viongozi wengine mbalimbali walijumuika
kumuunga mkono Katibu Mkuu kwenye ziara hii Muhimu.
No comments:
Post a Comment