Mfuko wa Maendeleo ya Jamii
(TASAF) ni moja ya nyenzo kuu ambazo serikali imezitumia katika kuhakikisha
inainua maisha ya Watanzania wa tabaka
la chini ambapo lengo kuu huwa ni kuinua hali ya maisha ya watu hao angalau
yafike katika tabaka la kati na wale wanaotumia vizuri fursa hii adimu hufika
mpaka tabaka la juu.
Mara baada ya kuanza
kufanikiwa kwa lengo mama la mfuko ambalo ni kutoa ruzuku isiyorejeshwa kwa
walengwa, Mfuko ulianza kuangazia miundombinu mbalimbali inayowazunguka
walengwa ambapo ulikusudia kupunguza au kuondoa changamoto zozote ambazo zitawafanya
walengwa kushindwa kuzalisha kutokana na ruzuku wanazopewa.
Wilaya ya Mkalama ni moja kati ya Maeneo ambayo mfuko
umedhamiria kuondoa kero mbalimbali
zilizokuwa zikiwakabili walengwa ambapo mchakato huu ulianza kwa kufanya
tathmini ya changamoto zilizoibuliwa na kupewa kipaumbele na jamii husika.
Katika kijiji cha Senene ,
Mfuko unaendelea na ujenzi wa bwawa kubwa la maji na Uanzishwaji wa Vitalu vya miti miradi ambayo ina thamani
ya shilingi 19,985,500.00 huku miradi
kama hiyo ikiwa imeanzishwa katika vijiji
vingine (gharama kwenye mabano) kama vile Lukomo (28,165,000.00),
Iguguno (63,735,000.00), Kidigida (19,529,500.00), Kidarafa (14,098,500.00), Mwanga (43,456,500.00), Nkalakala (22,168,500.00), Msiu (26,028,500.00),
Ipuli (25,762,500.00), Kinankamba (13,522,500.00), Mng’anda (8,733,500.00), Maziliga (12,907,000.00), Yulansoni (23,249,500.00), Kinyangiri (23,962,500.00), Ishenga (25,413,500.00), Singa (36,822,500.00), Iambi (19,047,500.00), Ilunda (34,018,000.00), Mbigigi (22,975,500.00), Dominic (18,881,500.00), Nkinto (32,493,500.00),
Makulo (15,081,500.00), Msingi (20,283,500.00), Ndurumo (10,497,500.00)
na Kijiji cha Kidii ambacho kinajengewa miradi kama hiyo kwa gharama ya
Shilingi 19,631,500.00.
Eneo jingine ambalo limemulikwa na Mfuko huo
Wilayani Mkalama ni Uondoaji wa
Makorongo katika vijiji vya Milade
utakaogharimu jumla ya shilingi 27,977,000.00, Malaja (30,662,000.00), Marera (18,155,500.00), Miganga (30,038,000.00 na ujenzi wa bwawa) na kijiji cha Nkungi mradi wenye thamani ya
shilingi 29,040,000.00 ikiwa ni
pamoja uanzishwaji wa Vitalu vya miti.
Mbali na miradi hiyo Mfuko umeangazia sekta ya
barabara za kijamii ambapo Kijiji cha Kitumbili kimewezeshwa ujenzi wa barabara
yenye urefu wa Km. 2.92 inayogharimu
shilingi 24,412,000.00, Msisai yenye
urefu wa Km 1.8 (16,445,000.00), Mgolombyo
yenye urefu wa Km. 1.38 (33,822,000.00),
Kinandili yenye urefu wa Km. 1.96
(17,744,000.00) na kijiji cha
Lyelembo kilichowezeshwa barabara yenye urefu wa Km. 4.16 inayogharimu
shilingi 33,822,000.00.
Kufuatia tatizo la ukosefu wa maji ambalo huwa
linayakumba maeneo mbalimbali katika Wilaya ya Mkalama, Mfuko umewezesha
uchimbwaji wa visima katika vijiji mbalimbali huku gharama hizo zikijumuisha
pia uanzishwaji wa Vitalu vya Miti kwa ajili ya kusaidia kutunza vyanzo hivyo
vya maji ambapo kijiji cha Tumuli kimewezeshwa ukarabati wa visima vitatu
vyenye thamani ya shilingi 16,848,500.00,
Kijiji cha Mkunguru Visima vitano vyenye thamani ya shilingi 11,531,000.00, Kijiji cha Ikungu visima
vitatu vyenye thamani ya Shilingi 18,622,500.00,
Kijiji cha Mgimba Visima nane vyenye thamani ya shilingi 9,254,500.00 na Kijiji cha Mntamba kilichowezeshwa visima vinne
vyenye thamani ya shilingi 20,834,500.00.
Jumla ya fedha ambazo serikali ya Tanzania kwa
ushirikiano Mkubwa na Benki ya Dunia imeweza kuzitumia katika miradi hiyo
Wilayani Mkalama ni shilingi 962,757,500.00
Pamoja na Serikali kutumia fedha nyingi kiasi hicho
katika miradi ya wananchi bado changamoto kubwa imekuwa ni utunzaji wa miradi
hiyo ambapo baadhi ya wananchi huwa wanaihujumu na kuwakosesha wengi huduma za
msingi hivyo katika kuunga mkono jitihada zote hizi zinazofanywa na Serikali ya
awamu ya tano Wilayani Mkalama ni vizuri wananchi wote wahahakikishe miradi hii
inatunzwa wakati wote ili iweze kuwa na manufaa kwa kizazi kilichopo na
vijavyo.
No comments:
Post a Comment