Hapa akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya. |
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya dokta Deogratius Masini akisoma taarifa fupi ya Idara ya Afya mbele ya Mhe: Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia na watoto. |
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe: Jackson Masaka akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mhe: Naibu waziri (Kulia). |
Hapa akikagua dawa na vifaa tiba vinavyopatikana katika kituo cha Afya Kinyangiri. |
Hapa akizungumza na wananchi wa kata ya Iguguno wakati akihitimisha ziara yake Wilayani hapa. |
Katika ziara hiyo, Kigwangala alianza kwa kutembelea
Zahanati ya Nduguti ambapo alitoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya Mkalama kuhakikisha anamaliza ujenzi wa Jengo la Kituo cha Afya cha Wilaya ndani ya Miezi sita.
“Kama mtaendelea kusubiri pesa za bajeti ili mkamilishe
jengo hili mtakuwa mnajichelewesha wenyewe kwa sababu kwa hatua lililofikia mna
uwezo wa kulimalizia kwa kutumia vyanzo vya ndani” Aliongeza Kigwangala.
Katika hatua nyingine, Mhe: Kigwangala alimsifu mhudumu
wa Zahanati hiyo, Josephine Mwakanyaga ambaye ndiye aliyekuwa akimpa maelezo
mbalimbali yanayohusu zahanati hiyo kwa uwezo mkubwa alionao katika uchambuzi
wa dawa na vifaa tiba.
“Huyu ni mhudumu mwenye uwezo mkubwa sana na anayejua
kitu anachofanya” Alisema Kigwangala.
Ziara ya Mhe: Kigwangala ilihitimishwa katika Zahanati
ya Iguguno ambapo alimsifu Mbunge wa jimbo la Mkalama Mhe: Allan Kiula na timu
yote ya Halmashauri ya Wilaya kwa hatua waliyolifikisha jengo jipya linalotarajiwa
kuwa kituo cha afya katika eneo hilo.
“Nawapongeza sana na ninawaahidi kuwaunga mkono kwa
kuhakikisha taratibu za usajili wa kituo hiki zinafanyika haraka sana ili
lianze kutumika mara moja mara baada ya kukamilika” Alimalizia Kigwangala.
Aidha katika kuunga mkono jitihada za Mhe: Kiula,
Kigwangala aliahidi kuchangia shilingi milioni moja ili kukamilisha ujenzi wa
Jengo hilo.
No comments:
Post a Comment